SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, September 28, 2010

Wapalestina watatu wauawa shahidi katika mashambulizi ya Israel
Sample Image

Wapalestina watatu wameuawa shahidi baada ya wanajeshi katili wa utawala wa Kizayuni wa Israel kufanya mashambulizi katika kambi ya wakimbizi ya al Bureij kusini mwa Ukanda wa Ghaza.
Msemaji wa jeshi la utawala wa Kizayuni amedai kuwa Wapalestina hao walikuwa wanajiandaa kurusha maroketi katika maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni.
Madai kama hayo hutolewa maafisa wa utawala wa Kizayuni kila wanapofanya jinai zao dhidi ya Wapalestina kama njia ya kuhalalisha jinai wanazofanya mara kwa mara katika maeneo ya Wapalestina hasa ya Ukanda wa Ghaza.
Itakumbukwa kuwa kabla ya utawala wa Kizayuni kufanya mashambulizi ya kikatili baina ya mwezi Disemba 2008 na Januari 2009 kwenye Ukanda wa Ghaza, moja ya madai yaliyotolewa na maafisa wa utawala huo dhalimu ili kuhalalisha jinai zao hizo za siku 22 ni eti kulipiza kisasi cha mashambulizi ya maroketi yanayotupwa na Wapalestina kutoka Ukanda wa Ghaza.
Zaidi ya Wapalestina 1,400 waliripotiwa kuuawa shahidi kwenye Ukanda wa Ghaza ambapo ukanda huo ulipata hasara ya zaidi ya dola bilioni 1.6 kutokana na mashambulizi hayo ya siku 22.

0 comments:

Post a Comment