SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, September 28, 2010

Muswada wa Obama wa kudhibitiwa Internet nchini Marekani
Sample Image

Rais Barack Obama wa Marekani anajiandaa kuwasilisha muswada wa kudhibitiwa matumizi ya Intaneti nchini humo.
Kwa mujibu wa muswada huo, maelezo binafsi ya watumiaji wa Intaneti ikiwa ni pamoja na barua-pepe zao na mitandao ya kijamii zitakuwa zinawafikia moja kwa moja polisi wa FBI.
Gazeti la New York Times limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, kama muswada huo utapitishwa, basi maelezo ya wanachama wa mitandao ya kijamii kama vile Facebook na Skype yatakuwa yanawafikia moja kwa moja polisi wa Marekani FBI itakapobidi.
Muswada huo unatarajiwa kuwasilishwa mbele ya Baraza la Congress la Marekani mwaka ujao wa 2011.
Maafisa usalama wa Marekani wanasema kuwa inabidi sheria na hatua mpya zichukuliwe kwa ajili ya kudhibiti na kuwekea mipaka matumizi na mawasiliano ya Intaneti nchini humo.
Lakini baadhi ya weledi wa mambo wameelezea wasiwasi wao kuwa hatua hizo mpya zitapelekea watu wenye nia mbaya kupenya ndani ya barua-pepe za watu binafsi na kufanya uhalifu na uharibifu. 

0 comments:

Post a Comment