Mamia kwa maelfu wa wananchi wa Iran wamemiminika katika barabara zote kuu za jiji Tehran leo hii baada ya sala ya Ijumaa katika maandamano ya kulaani kitendo cha kuchomwa moto Qur'ani tukufu nchini Marekani. Wakiungana na baadhi ya maafisa wa ngazi za juu wa Serikali, waandamanaji hao waliokuwa wamebeba mabango na maberamu yaliyokuwa na ujumbe wa kuwatakia maangamizi Wamarekani na Wazayuni wenye misimamo ya kufurutu ada, walisikika wakitoa kauli za kumlaani Kasisi Terry Jones wa kanisa la Florida, ambaye ndiye kaja na fikra hiyo ya kiwendawazimu ya kuchomwa moto Qur'ani Tukufu. Licha ya kuwa kasisi huyo kwa mashinikizo ya ulimwengu wa Kiislamu baadaye aliakhirisha azma yake ya kijuba, lakini yenye ndiye anayehesabiwa kuwa ndiye aliyewachochea waandamanaji wa Kimarekani kurarua na kuchoma moto nakala za Kitabu hicho kitukufu wakati wa kumbukumbu za mashambulizi yenye utata mwingi ya Septemba 11, 2001, yaliyopelekea maelfu ya Wamarekani kufariki dunia. Kitendo hicho cha kijuba kimepelekea kufanyika maandamano ya mamilioni ya Waislamu kote ulimwenguni kulaani kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu na matukufu mengine ya Kiislamu.
Friday, September 17, 2010
Wananchi wa Iran waandamana kulaani kuchomwa moto Qur'ani Tukufu Marekani
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Friday, September 17, 2010
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
0 comments:
Post a Comment