Chama tawala cha ANC nchini Afrika Kusini kinatazamiwa kufanya mkutano muhimu juma lijalo ambao utajadili hatima ya Rais Jacob Zuma na namna ya kuuratibu upya mfumo wa uchumi wa nchi hiyo. Mkutano huo wa Baraza la Taifa la chama hicho, utafanyika kuanzia siku ya Jumatatu na kumalizika siku ya Ijumaa mjini Durban. Baraza hilo litajadili miongoni mwa ajenda nyiingine, namna ya kuimarisha sera za chama hicho tawala na mikakati mipya ya kuimarisha uchumi wa nchi hiyo ambao ndio mkubwa zaidi barani Afrika. Mkutano huo umekuja katika hali ambayo, baadhi ya wapambe wa Rais Jacob Zuma wametishia kutomuunga mkono katika kugombea muhula wake wa pili. Aidha, baraza hilo linatazamiwa kujadili kadhia ya wafanyakazi wa sekta ya umma ambao wamekuwa katika mgomo wa kutaka nyongeza ya mishahara yao na marupurupu ya nyumba siku chache zilizopita.
Friday, September 17, 2010
ANC kufanya mkutano kuhusu Rais Zuma na hali ya uchumi Afrika Kusini
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Friday, September 17, 2010
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
0 comments:
Post a Comment