SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, September 22, 2010

Tume ya Uchaguzi ya Nigeria yataka tarehe ya uchaguzi mkuu kusongezwa mbele

Tume ya Uchaguzi ya Nigeria imeviomba vyama vya kisiasa kukubali tarehe ya uchaguzi kusongezwa mbele ili kuipa nafasi ya kutosha ya kuweza kuandaa uchaguzi huru na wa haki. Mwenyekiti wa tume hiyo Attahiru Jega amesema ni wazi kwamba Januari 22 haitokuwa tarehe muafaka kwa uchaguzi mkuu kufanyika kwani hadi sasa matayarisho bado yako mbali na kwamba tume yake inahitaji miezi miwili au mitatu zaidi ili iweze kuandaa uchaguzi utakaokubaliwa na pande zote. Jega amependekeza uchaguzi huo ufanyike Aprili mwaka ujao. Huku hayo yakijiri ufa ndani ya chama tawala nchini humo PDP unaendelea kupanuka baada ya Rais Goodluck Jonathan kutangaza nia yake ya kugombea urais jambo ambalo ni kinyume na makubaliano yasiyo rasmi ya chama hicho. Mgombea urais kwa tikiti ya PDP anapaswa kutoka eneo la kaskazini lenye Waislamu wengi kwa mujibu wa makubaliano hayo. Jonathan anayetoka eneo la kusini lenye Wakrito wengi aliingia uongozini mapema mwaka huu baada ya kufariki dunia Umaru Yar'Adua kutoka eneo la Kaskazini.

0 comments:

Post a Comment