Mkuu wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema leo kuwa vikosi mbali mbali vya ulinzi vimejiandaa barabara kukabiliana na tishio lolote dhidi ya nchi hii. Meja Jenerali Hassan Firouzabadi ameyasema hayo kwenye sherehe za kuanza rasmi wiki ya kitaifa ya jeshi na ulinzi humu nchini. Firouzabadi amesisitiza kuwa askari wa Kikosi cha Kulinda Mapinduzi ya Kiislamu pamoja na wa Jeshi la Taifa kwa pamoja wamejiimarisha zaidi hii leo kuliko wakati wa huko nyuma. Wiki ya Kitaifa ya Ulinzi huanza kila mwaka Septemba 22 ili kukumbuka kuanza kwa vita vya kulazimishwa vilivyodumu kwa miaka minane kati ya Iran na Iraq kuanzia mwaka 1980 - 1988. Mkuu wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa vita hivyo vya kulazimishwa vilivyochochewa na Marekani na waitifaki wake vimelifanya jeshi la Iran na wananchi kwa ujumla kuwa macho na kujiandaa barabara kukabiliana na adui.
Wednesday, September 22, 2010
Jeshi la Iran lasema liko tayari kukabiliana na tishio lolote
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Wednesday, September 22, 2010
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
0 comments:
Post a Comment