Mtoto wa kiume wa mwisho wa kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong-il, ameteuliwa katika nyadhifa mbili za juu nchini humo. Kijana huyo Kim Jong-un aliye na chini ya miaka 30 hajawahi kuhudumu katika afisi yoyote ya umma nchini humo na hatua ya kumteua inaonekana kuwa maandalizi yake kuchukuwa wadhifa wa baba yake kama kiongozi wa nchi.
Uongozi wa Korea Kaskazini
Kuchambua uongozi wa Korea Kaskakazini wenye usiri mwingi sio kazi rahisi, lakini inaonekana wazi kuwa Kim Jong-Un sasa ameteuliwa kuchukua uongozi wa nchi hiyo.
Hii inashiria mwanzo wa kipindi cha mpito ambacho muda wake bado haujajulikana.
Babake, Kim Jong-Un anaugua na inaaminika kuwa alipooza mara mbili , mwaka wa 2008. Uamuzi wake wa kuanzisha kipindi hiki cha mpito ni ishara kwamba hali yake ni mbaya.
Kim Jong - Un ni nani?
Machache yanajulikana kuhusu Kim Jong-Un tangu wakati alipokuwa akisomea nchini Uswizi. Hata umri wake haujulikani na inadhaniwa kuwa ana umri wa miaka 27.
Hali ya wasiwasi inazingira mipango ya kumrithi Kim Jong-Il. Huenda Kiongozi huyo wa kikomunisti akaondoka madarakani polepole au huenda kiongozi mwenye ushawishi ,mwenye cheo cha tatu cha juu katika utawala huo, Jang Song-Thaek, ambaye pia ni mwenyekiti wa tume kuu ya kitaifa ya ulinzi, akafanywa kuwa mshauri wa kijana Kim Jong-Un?
Swali lingine ni kuhusu shughuli ya kumuandaa kijana Un. Je! itachukua muda gani kabla ya yeye hatimaye kushikilia wadhifa huo?
Hii ndio sababu waangalizi wa nje wa masuala ya Korea Kaskazini wana wasiwasi sana.
Korea Kaskazini bado inatawaliwa kijeshi. Kama kutafanyika mabadiliko machache katika tume kuu ya jeshi la nchi hiyo, basi huenda uhusiano na nchi za nje usibadilike.
0 comments:
Post a Comment