White House imetaka mshukiwa wa shambulizi la kigaidi dhidi ya ndege ya abiria katika anga ya Lockerbie Abdul Basit Al-Megrahi arejeshwe jela nchini Scotland. John Brennan Mshauri wa Rais Barack Obama katika masuala ya kupambana na ugaidi amesema kwamba kuachiliwa huru al- Megrahi ni makosa na ameitaka serikali ya Uingereza imrudishe jela. Mwaka 2001 Al-Megrahi alihukumiwa kifungo cha miaka 27 jela lakini mahakama ya Scotland ilimuachia huru Agosti 20 mwaka jana baada ya afya yake kudhoofika kupindukia kutokana na maradhi ya kansa. Nchi za Magharibi zinahofia kwamba sherehe za kutimia mwaka mmoja tangu mshukiwa huyo aachiliwe huru zinaweza kuamsha hasira za familia za wahanga wa tukio hilo lililotokea mwaka 1988 na kusababisha vifo vya watu 259 wengi wakiwa raia wa Marekani.
Saturday, August 21, 2010
Marekani yatoa wito wa kurejeshwa jela mshukiwa wa shambulizi la Lockerbie
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Saturday, August 21, 2010
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
0 comments:
Post a Comment