Kiwanda cha kwanza cha kuzalisha nishati ya nyuklia cha Iran ambacho kiko katika mji wa bandari wa Bushehr kinatarajiwa kuanza kuwekwa fueli ya nyuklia leo Jumamosi. Hafla za kuwekwa fueli katika kituo hicho zitahudhuriwa na Ali Akbar Salehi Mkuu wa Taasisi ya Atomiki ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pamoja na Dergei Kiriyenko Mkuu wa Taasisi ya Nyuklia ya Russia. Fueli ya nyuklia itakuwa ikisafirishwa hadi katika kiwanda hicho cha nyuklia cha Bushehr chini ya usimamizi wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA). Kuanza kufanya kazi kiwanda hicho ni hatua muhimu katika jitihada zinazofanywa na Iran za kuzalisha nishati inayotokana na nyuklia. Inatarajiwa kuwa wananchi wa Iran wataanza kufaidika na nishati iliyozalishwa kutokana na nyuklia miezi miwili au mitatu baada ya kuanza kazi kiwanda hicho.
Saturday, August 21, 2010
Kiwanda cha nyuklia cha Bushehr Iran kuanza kazi leo
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Saturday, August 21, 2010
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
0 comments:
Post a Comment