SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, August 21, 2010


CCM YAZINDUA RASMI KAMPENI ZAKE VIWANJA VYA JANGWANI LEO!!

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Cham Cha Mapinduzi Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia wanaCCM wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho uliofanyika kwenye viwanja vya Jangwani jijini Dar es salaam leo. Mh rais amezungumzia mambo mengi ambayo yamefanywa na CCM chini ya utawala wake na kuwaambia wana CCM kuwa wanatakiwa kuiongezea muda mwingine CCM ili iweze kuendeleza yote ambayo yanatakiwa kukamilika katika kipindi cha miaka mitano ijayo kwa kutekeleza Sera na Ilani ya Chama cha Mapinduzi. Baada ya kuzindua rasmi Kampeni hizo hivi sasa zitaanza katika majimbo yote nchini kwa urais ubunge na udiwani na uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu nchini kote.
Mgombea Mwenza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. Mohamed Ghalib Bilal naye alipata wasaa wa kuongea na wanaCCM katika uzinduzi huo.
Rais wa Serikali ya Mapindzi Zanziba na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi anayemaliza muda wake Dr Amani Abeid Karume akihutubia mamia ya mashabiki na wanachama wa chama cha Mapinduzi wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho leo.
Mgombea Mwenza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Mohamed Bilal na Mgombvea urais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dr. Alli Mohamed Shein na rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Benjamin William Mkapa nao wakiondoka kwenye eneo la mkutano mara baada ya uzinduzi wa kampeni hizo.
Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete akiondoka mara baada ya kuzinduz rasmi kampeni za chama hicha kwa nchi nzima katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Jangwani Jijini Dar es salaam leo.
Wagombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi Dr Jakaya Kikwete na Dr Mohamed Ghalib Bilal wakiondoka kwenye eneo la mkutano mara baada ya uzinduzi rasmi wa kampeni hizo kwenye viwanja vya Jangwani jijini Dar es salaam.
Kundi la TOT likiongozwa na mwanamuziki Nguli wa Muziki wa Kwaya na kada wa Chama cha Mapinduzi Kapteni John Komba (MB) likitumbuiza wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho leo.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Marlow na kundi lake wakitumbuiza wakati wa uzinduzi wa kampeni9 hizo leo kwenye viwanja vya Jangwani.
Mwandishi mwandamizi wa gazeti la Habari Leo Oscar Mbuza kushoto akiwa amekaa na waandishi wengine kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia hotuba za viongozi katika uzinduzi wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi CCM uliofanyika leo viwanja vya Jangwani jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM wakiwa wameshikilia bango kubwa lenye picha ya mgombea urais wa chama hicho Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM wakiwa wamefureika kwenye mkutano wa Uzinduzi wa kampeni za Chama hicho uliofanyika leo mchana kwenye viwanja vya Jangwani ukihutubiwa na wagombea urais wa Chama hicho Rais Jakaya Kikwete na Mgombea Mwenza Dr. Mohamed Ghalib Bilal.

0 comments:

Post a Comment