Jana ilikuwa ni Patashika nguo kuchanika katika uwanja wa MASAB TANK HYDERABAD INDIA mtanange mkali kati ya Timu ya Tanzania na Sudan katika kinyanganyiro kinachoitwa RAMADHAN TORNAMENT.
Timu hizi mbili zina upinzani wa muda mrefu kwa miaka mingi,na Timu ya Sudan ni washindi wa mashindano haya kwa miaka kadhaa.Hatimaye jana njozi zao hizo za ushindi wa miaka kadhaa katika mashindano haya zilipobadilishwa na vijana machachari wa timu ya Tanzania na kufanikiwa kuwatoa katika kinyanganyiro hicho baada ya kuchabangwa bao 2 kwa 1.Bao la kwanza kwa upande wa Tanzania lilifungwa na msakata kabumbu machachari Said Omar Mihala aka Young Halla na bao la pili Sudan walijifunga wenyewe baada ya vuta nikuvute iliyofanywa na Tanzania golini mwao na hatimaye mpira kuingia nyavuni,na sudan wakajipatia bao la kifutia machozi.
Hadi mwisho wa mechi hiyo Tanzania walitoka kifua mbele kwa kuifunga Sudan 2 kwa 1.
Timu ya Tanzania jana imeweza kupata nafasi ya kuingia nusu fainali katika mashindano hayo.
Timu ya Tanzania jana imeweza kupata nafasi ya kuingia nusu fainali katika mashindano hayo.
Leo saa mbili na nusu usiku huu ilikuwa vijana wa Tanzania waingie dimbani kupambana na timu ya Afghanistan,
Hatimaye mechi hiyo imeahirishwa na kusogezwa mbele siku na tarehe bado haijapangwa kutokana na mvua kubwa sana iliyokuwa ikinyesha mjini hapa na kusababisha mtanange huo ushindwe kufanyika kutokana na uwanja huo kujaa maji.
Hivyo basi uongozi wa TSAH unawaomba wanajumuiya kuwa wastahimilivu hadi hapo mtapotangaziwa tena siku na tarehe ya mechi hiyo, mnaombwa kujitokeza kwa wingi bila kukosa kuishangilia timu
yenu msisahau kuja na mavuvuzela.
Mungu ibariki Tanzania,Watanzania TSAH,na Watu wake,Amin.
Mungu ibariki Tanzania,Watanzania TSAH,na Watu wake,Amin.
Imeandikwa na ALLY S. MGIDOS.
0 comments:
Post a Comment