Rais mpya wa Ujerumani Christian Wulff
Mgombea wa muungano wa serikali
inayongozwa na Kansela Angela Merkel, Christian Wulff jana usiku
amechaguliwa kuwa rais mpya wa Shrikisho la Ujerumani.
Uchaguzi huo ulilazimika kurudiwa mara tatu, kabla ya Bwana Wulff
kupata idadi ya kura za bunge la shirikisho zinazomruhusu kuchaguliwa
kuwa rais.
Christian Wulff hatimaye alifanikiwa kupata idadi hiyo ya kura dhidi
ya mgombea wa mrengo wa kati kushoto anayeungwa mkono na upinzani
Joachim Gauck, na Spika wa bunge, Nobert Lammert kumtangaza kuwa rais
mpya wa Ujerumani.
Kurejewa mara tatu kwa uchaguzi huo, kunaonekana kama ni pigo kwa
Kansela Merkel ambaye kura za maoni za hivi karibuni zimeonesha kupungua
kwake umaarufu na kuzua wasi wasi kuwa ameshindwa kuidhibiti serikali
ya muungano na chama cha FDP kinachowapendelea wafanyabiashara.
Christian Wulff anachukua nafasi hiyo ya urais wa Ujerumani ambayo ni
ya heshima kutoka kwa Horst Koehler ambaye kujiuzulu kwake ghafla mwezi
mmoja uliyopita lilikuwa ni pigo lingine kwa Kansela Merkel na serikali
yake.
Mwandishi:Aboubakary Liongo
0 comments:
Post a Comment