Iran kuisaidia Kenya kujenga nyumba za kisasa kwa bei nafuu
Shirika moja la Iran limeafiki kufadhili ujenzi wa nyumba takribani 3000 nchini Kenya.Kwa mujibu wa mkataba wa maelewano uliotiwa saini kati ya Shirika la Mahun la Iran na Shirika la Taifa la Nyumba la Kenya-NHC- shirika hilo la Iran litatoa takribani shilingi bilioni sita kujenga nyumba hizo kwa teknolojia ya kisasa na ambazo watauziwa wananchi wa Kenya kwa bei nafuu. Makubaliano hayo yametiwa saini mjini Nairobi jana katika kikao kilichohudhuriwa na balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Kenya Dr Seyyed Ali Sharifi. Akizungmza katika kikao hicho Balozi Sharifi amesema kwa mtazamo wa Iran Kenya si lango la Afrika Mashariki tu bali ni lango la bara zima la Afrika
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akaribisha mazungmzo ya nyuklia ya Iran
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amekaribisha wazo la kuanza tena mazungmzo ya nyuklia kati ya Iran na Kundi la Vienna.
Msemaji wa Katibu Mkuu Martin Nesirky amewaambia waandishi habari mjini New York kuwa Ban daima amekuwa akiunga mkono kuanza upya mazungmzo. Kundi la Vienna linajumuisha Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA, Russia, Ufaransa na Marekani. Wakati huo huo Balozi wa Iran katika IAEA mjini Vienna Ali Asghar Sultaniyeh, jana alimkabidhi mkuu wa wakala huo, Yukia Amano, barua rasmi ya Iran ambapo Tehran imetangaza kuwa tayari kufanya mazungumzo na Kundi la Vienna kuhusu ubadilishanaji mafuta ya nyuklia kwa ajili ya kinu cha nyuklia cha Tehran.

0 comments:
Post a Comment