SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, July 22, 2010

Serikali ya Marekani yakiri kuwa utumwa bado upo nchini humo
Sample Image

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imetoa ripoti ikikiri kwa mara ya kwanza kwamba utumwa bado unashuhudiwa nchini humo katika sura ya kisasa.

Duru za habari za Marekani zimeandika kuwa miaka 150 baada ya kufutwa utumwa nchini Marekani Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo imethibitisha kwamba biashara ya kuuza na kununua wanadamu kama milki nyingine ingali inafanyika nchini humo. 

Ripoti ya mwaka huu wa 2010 ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imechunguza kwa ujumla magendo ya wanadamu na hatua za kisheria kuhusu suala hilo nchini Marekani. 

Kituo cha habari cha In These Times cha Marekani kimesema kuwa miongoni mwa sababu za kuwepo utumwa wa kisasa ni ukosefu wa usawa katika nchi mbalimbali suala ambalo linazidishwa na masuala ya kiuchumi. Mkurugenzi wa sera wa Muungano wa Kufuta Utumwa na Utoroshaji wa Wanadamu wenye makao yake mjini Los Angeles Stephanie Richard, amethibitisha takwimu za wahamiaji wanaoingizwa Marekani kwa visa sahihi na kusema kuwa wahamiaji hao wanatumiwa kama watumwa
. 
Clegg: Mashambulizi ya Marekani dhidi ya Iraq yalikuwa kinyume cha sheria

Sample ImageNaibu Waziri Mkuu wa Uingereza Nick Clegg amesema kuwa mashambulizi ya Marekani na waitifaki wake dhidi ya Iraq mwaka 2003 yalifanyika kinyume cha sheria. Clegg ambaye alikuwa akizungumza bungeni kwa niaba ya Waziri Mkuu David Cameron aliyeko safari nchini Marekani, amelumbana vikali na Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Uingereza Jack Straw bungeni hapo akisema atakuja kuhukumiwa kutokana na mchango wake katika maamuzi yaliyokuwa na maafa makubwa kushinda yote ambayo ni kuivamia kijeshi Iraq kinyume cha sheria. 
Matamshi hayo na Naibu Waziri Mkuu wa Uingereza ambaye chama chake cha Liberal Democrats kinaunda muungano unaotawala pamoja na chama cha Conservative, yanaiweka serikali ya sasa ya London chini ya mashinikizo makubwa na kudhihirisha tofauti ya sera za vyama hivyo viwili.
Inakadiriwa kuwa watu milioni moja wamefariki dunia kutokana na mashambulizi ya kijeshi yaliyoongozwa na Marekani na Uingereza na waitifaki wao dhidi ya Iraq tangu mwaka 2003.

0 comments:

Post a Comment