Umoja wa Afrika wakiri askari wake wanashambulia maeneo ya raia Somalia
Umoja wa Afrika umekiri katika ripoti yake ya siri kwamba askari wake wanaolinda amani nchini Somalia wanashambulia ovyo maeneo ya raia mjini Mogadishu. Shirika la habari la Associated Press limefichua kwamba Umoja wa Afrika umesema katika ripoti ya siri iliyochapishwa mwezi Mei mwaka huu kwamba ofisi ya kikosi cha Umoja wa Afrika nchini Somalia haikutoa umuhimu kwa suala la kushambuliwa ovyo maeneo ya raia mjini Mogadishu. Ripoti hiyo imetahadharisha kwamba askari wa Umoja wa Afrika watapoteza uungaji mkono wa raia wa Somalia iwapo wataendelea kushambulia maeneo ya raia. Itakumbukwa kuwa kundi la al Shabaab la Somlia lilitumia hoja ya kushambuliwa raia wa Mogadishu kuhalalisha mashambulizi yake ya karibu wiki mbili zilizopita mjini Kampala ambayo yalisababisha vifo vya watu wasiopungua 76.
0 comments:
Post a Comment