Polisi wamesema, padri wa Rwanda
anayeshutumiwa kusaidia kupanga mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 katika
nchi yake ya asili ameshikiliwa nchini Uganda.
Jean-Bosco Uwinkindi alikamatwa baada ya kuingia
Uganda ya magharibi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Bw Uwinkindi alishtakiwa mwaka 2001 na mahakama
inayoungwa mkono na umoja wa mataifa inayoshughulikia mauaji ya kimbari
na uhalifu dhidi ya binadamu.
Takriban Watutsi 800,000 na Wahutu wenye msimamo
wa wastani waliuliwa na wanamgambo wa Kihutu katika mauaji ya siku 100
mwaka 199
Uchinjaji kanisani
Polisi ya Uganda ilitangaza siku ya Ijumaa kuwa
Bw Uwinkindi aliwekwa rumande siku ya Jumatano.
Polisi wamesema mshukiwa huyo alisakwa kwa siku
mbili kabla ya kutiwa kizuizini.
Gazeti la Daily Monitor limeripoti kuwa Bw
Uwinkindi aliingia Uganda kwa kutumia jina tofauti na alikuwa akijaribu
kununua ardhi ili aweke makao yake hapo.
Kushtakiwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu
kwa Rwanda (ICTR) inasema Bw Uwinkindi alikuwa mchungaji katika kanisa
la Pentekosti karibu na mji mkuu wa Rwanda, Kigali mwaka 1994.
Anashutumiwa kwa kuamuru kuuawa kwa Watutsi,
wakiwemo wanawake na watoto, baada ya kuomba hifadhi kwenye kanisa lake.
Waendesha mashtaka wanadai uchunguzi uliofanyika
baada ya mauaji ya kimbari, takriban maiti 2,000 zilipatikana karibu na
kanisa hilo.
Mpaka alipokamatwa, Bw Uwinkindi alikuwa
miongoni mwa washukiwa 11 waliokuwa wakisakwa na ICTR.
Marekani iliahidi kutoa zawadi ya dola za
kimarekani milioni tano kwa yeyote atakayetoa taarifa zitakazosaidia
kukamatwa kwake. Haijfahamika wazi iwapo kuna yeyote atakayedai zawadi
hiyo nono.
Elly Womanya, naibu mkurugenzi wa ofisi ya
upelelezi ya Interpol mjini Kampala, amesema mshukiwa huyo atapelekwa
ICTR Arusha, Tanzania, haraka iwezekanavyo.
Bw Uwinkindi ni mshukiwa wa pili anayehusishwa
na mauaji ya kimbari Rwanda kukamatwa Uganda katika kipindi kisichozidi
mwaka mmoja.
Mwezi Oktoba 2009, Idelphonse Nizeyimana,
aliyekuwa mkuu wa upelelezi mwenye asili ya Kihutu, alikamatwa mjini
Kampala.
0 comments:
Post a Comment