Mfuko wa Fedha wa Kimataifa: Uchumi wa Tanzania unakua kwa kasi
Mfuko wa Fedha wa Kimataifa IMF umetangaza kuwa uchumi wa
Tanzania
unakuwa kwa kasi isiyo ya kawaida. IMF imeongeza kuwa uchumi wa nchi
hiyo utakuwa na kufikia asilimia 6.7 mwaka ujao kinyume na makadirio ya
hapo awali ya asilimia 6.2. Mwaka uliopita uchumi wa Tanzania ulikuwa
kwa asilimia 6. Taarifa ya IMF imesema kuwa hali hiyo ya ukuaji wa kasi
wa uchumi wa Tanzania imetokana na kupungua kwa bei ya vyakula kutokana
na kuongezeka kwa mazao ya vyakula hivyo mwaka uliopita.
*************************
Bunge la Kenya lapitisha sheria inayoipa serikali uwezo wa
kudhibiti bei |
|
|
|
Bunge la Kenya
limeidhinisha sheria inayoipa serikali uwezo wa kudhibiti bei za bidhaa
muhimu kama vile chakula na mafuta ya petroli. Sheria hiyo ambayo
ilikuweko huko nyuma lakini ikaondolewa katika mwongo wa 90 itaipa
serikali nguvu ya kuzuia wafanya biashara kupandisha ovyo bei za bidhaa
muhimu kama wanavyofanya hivi sasa. Mwanabiashara atakayepatikana
akiongeza bei za bidhaa bila ya idhini ya serikali atachukuliwa hatua
kali za kisheria. Serikali imekaribisha hatua hiyo ikisema kuwa
waliokuwa wakijitajirisha kwa njia isiyo ya halali sasa hawana tena
nafasi hiyo. Hata hivyo mawaziri wengi wa serikali wamepinga sheria hiyo
wakisema kuwa inatishia mustakabali wa uchumi wa nchi hiyo. |
|
|
|
|
|
|
0 comments:
Post a Comment