SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, June 17, 2010

Forlan awanyamazisha South Africa

Diego Forlan (C) of Uruguay celebrates after scoring the opening 
goal with team mate Jorge Fucile and Alvaro Pereira
   Diego Forlan kwa mara ya kwanza anyamazisha umauti South Africa 2010 toka mashindano ya kombe la Dunia kuanza na  ushambuliaji wake wa kushangaza kwa kuifunga South Afrika mabao 2 na bao la 3 la ushindi lilifungwa na mchezaji Alvaro Pereira kufanya jumla ya mabao 3-0.Mechi iliyofanyika katika uwanja wa  Tshwane/Pretoria - Loftus Versfeld Stadium
   Katika mechi hiyo mchezaji Diego Forlan alichaguliwa kuwa mchezaji bora.
Afrika Kusini yanyukwa na Urugua
    Matumaini ya Afrika Kusini kufanya vyema katika mashindano ya Kombe la Dunia yanayofanyika katika ardhi yake, yamefifia baada ya kufungwa 2-0 na Uruguay katika mechi iliyochezwa uwanja wa Loftus Versfeld mjini TShwane au Pretoria.
   Afrika Kusini walianza kwa gonga zilizowapatia sare kwenye mechi ya ufunguzi dhidi ya Mexico, lakini kadri muda ulivyokuwa ukisonga mbele, walianza kumeguka na kushindwa kuhimili vishindo na njama za washambuliaji wa Uruguay.
   Kunako dakika ya 24, Diego Forlan aliachia mkwaju wa mbali ambao ulienda kushoto kwa mlinda mlango Itumeleng Khune ambaye hata hakuweza kuruka kujaribu kuufikia.Alikuwa ni mlinda mlango Itumeleng Khune, aliyebadilisha taswira ya matumani ni ya Afrika Kusini wakati mwamuzi Massimo Bussaca alimwonyesha kadi nyekundu kwa kufanya madhambi ndani ya 18 na kutoa penati ambayo Diego Forlan aliitumia kupachika goli la pili katika dakika ya 80.
   Kwa matokeo hayo, Afrika Kusini watatakiwa kuifunga Ufaransa katika mechi ya mwisho na Mexico itoke sare na Ufaransa kisha mechi ya mwisho Mexico iifunge Uruguay. Hayo ni mambo ya pata potea, lakini katika hali halisi itabidi Afrika Kusini wawe watazamaji baada ya hatua ya awali.










0 comments:

Post a Comment