Siku ya Watoto
Afrika ilivyoadhimishwa leo Dar
Watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu wanaotoka
Kikundi cha New Hope Family Street Children jijini Dar es Salaam,
wakiandamana huku wakiwa na mabango yenye ujumbe unaoitaka Jamii na
Serikali kuwajali kwa kuwapatia haki yao ya kupata elimu na maisha
mazuri. Watoto hao ambao asilimia kubwa wanaishi mitaani katikati ya
Jiji walifanya maandamano hayo kivyao baada ya kutoalikwa kwenye
shughuli mbalimbali za maadhimisho ya Siku ya Mtoto Afrika leo. Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii wa Wizara ya Maendeleo
ya Jamii, Jinsia na Watoto, Leoni Msimbe (kulia) akiangalia michoro
ilichorwa kwenye kuta za jengo la Watoto Muhimbili kwa msaada wa OTIS.
Kushoto ni Esther Micahael ambaye ni Mhandisi Mauzo wa OTIS Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii wa Wizara ya Maendeleo
ya Jamii, Jinsia na Watoto, Leoni Msimbe (kulia), akiwalisha keki watoto
wanaopata matibabu kwenye Hospitali ya Muhimbili jijini Dar leo.Watoto wanaopata matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dar es Salaam, wakipuliza kuzima mishumaa kwenye keki iliyoandaliwa wakati wa uzinduzi wa michoro iliyochorwa kwa msaada wa Kampuni inayotengeneza lifti ya Otis kwenye Jengo la Watoto la MNH, ikiwa ni moja ya shamrashamra ya maashimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika jijini leo
(kushoto) akigawa zawadi kwa watoto wakati wa
hafla hiyo.. Michuzi blog
0 comments:
Post a Comment