Kiswahili Radio.
Monday, May 24, 2010
Wananchi wa Iraq wanazidi kuwa wahanga wa silaha hatari za Marekani
Wananchi wa
Iraq wamekuwa wahanga wa makombora yenye urani iliyodhoofishwa
yaliyotumiwa na majeshi ya Marekani nchini Iraq. Taarifa ya Wizara ya
Afya ya Iraq inasema kuwa, maradhi ya saratani yameongezeka kwa zaidi ya
mara tatu nchini humo, huku wengi wa watoto wanaozaliwa wakiwa na
upungufu wa baadhi ya viungo vya mwili. Taarifa hiyo imeeleza kuwa kati
ya mwaka 2005 hadi 2007, maradhi ya kansa kwa watoto wa Kiiraqi
yameongezeka kwa zaidi ya mara tatu. Taarifa hiyo imeongeza kuwa, mada
za sumu za silaha za Marekani zitaendelea kuleta athari mbaya kwa afya
ya wananchi wa Iraq hadi miaka hamsini ijayo. Wakati huohuo, taarifa
kutoka Iraq zinasema kuwa, idadi ya watoto yatima nchini Iraq
imeongezeka na kufikia milioni tano hali ambayo imeshadidisha matatizo
ya kiroho na kisaikolojia. Taarifa zinasema kuwa, watoto hao wamekuwa
yatima baada ya wazazi wao kuuawa, pale majeshi ya Marekani yalipoanza
mashambulizi nchini humo yapata miaka saba iliyopita.
Kiswahili Radio.
Kiswahili Radio.
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Monday, May 24, 2010
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
0 comments:
Post a Comment