SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, May 24, 2010

Israel yakana kuisaida A Kusini kinuklia

Rais wa Israel Shimon Peres amekana ripoti inayodai kulikuwa na makubaliano ya silaha za kinyuklia baina ya Israel na Afrika Kusini wakati ililipokuwa ikifuata siasa za ubaguzi wa rangi.
Shimon Peres
Shimon Peres
 Gazeti la The Guardian limeripoti, nyaraka zinazotakiwa kuchapishwa katika kitabu kipya zinaonyesha Israel ilikubali kuipa Afrika Kusini silaha za kinyuklia mwaka 1975.
Bw Peres alikuwa waziri wa ulinzi kwa wakati huo na alitajwa kwenye ripoti ya gazeti hilo.
Taarifa hizo zimetolewa huku wasiwasi juu ya silaha za nyuklia eneo hilo zikiongezeka.
Msemaji wa Bw Peres, Ayelet Frisch, amekana kuwepo na majadiliano baina ya nchi hizo mbili.
Mtandao wa habari wa Israel umemnukuu Bi Frisch akisema, " Tunasikitika kuwa gazeti hilo halikuona umuhimu wa kupata kauli kwa maafisa na kufanya tathmini na vyanzo vengine vya Israel."

'Utata'
The Guardian limeripoti nyaraka za siri za awali, ziliofichuliwa na msomi wa Marekani Sasha Polakow-Suransky, alitoa nyaraka ya kwanza kama ushahidi wa kuwepo kwa silaha za kinyuklia za Israeli.
Israel inafanya kazi chini ya sera yenye utata juu ya mpango wake wa kinyuklia, lakini mwaka 1986 fundi wa masuala ya kinyuklia wa Israel Mordechai Vanunu alitoa taarifa za kuwepo kwa kinu cha nyuklia huko Israel.
Shirikisho la wanasayansi wa Marekani wanakadiria kuwa Israel huenda ikawa imetengeneza hadi silaha za nyuklia 200.
The Guardian nalo limeripoti kuwa nyaraka hizo zinaweza kudhoofisha madai yeyote yatakayotolewa na Israel kwamba ni nchi inayofuata sheria na inaweza kuaminiwa kuwa na silaha za nyuklia, wakati Iran haiwezi.
Madai ya makubaliano hayo pia yanaashiria uzito wa uhusiano baina ya serikali ya Israel na Afrika Kusini iliyokuwa ikifuata siasa za kibaguzi.
BBC Swahili

0 comments:

Post a Comment