SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, May 27, 2010

Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel washambulia tena Ghaza

Sample ImageMuda mchache baada ya ndege za utawala wa Kizayuni wa Israel kufanya mashambulizi katika Ukanda wa Ghaza, wanajeshi wa nchi kavu wa utawala huo dhalimu wamewashambulia kwa risasi wananchi wa Palestina wasio na ulinzi katika ukanda huo.
Hii ni kusema kuwa, Wapalestina 17 wameripotiwa kujeruhiwa wakiwemo watoto wadogo katika mashambulizi ya jana ya ndege za utawala wa Kizayuni.
Vibarua watatu wa Kipalestina nao wameripotiwa kujeruhiwa vibaya kwa risasi za wanajeshi wa nchi kavu wa Israel.
Tangu mwaka 2007, Ukanda wa Ghaza umezingirwa kwa kila upande na utawala wa Kizayuni ambao unazuia kuingia na kutoka chochote katika ukanda huo.
Hivi sasa wakazi wa Ghaza wanakabiliwa na matatizo mengi yakiwemo ya upungufu mkubwa wa chakula na madawa huku madola ya kibeberu yakiangalia kwa macho tu jinai hizo za Wazayuni. Kiswahili Radio






0 comments:

Post a Comment