Daktari mmoja
wa Kinyarwanda ametiwa mbaroni na maafisa wa Ufaransa kwa tuhuma za
kuhusika katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 yaliyopelekea kuuawa
karibu watu milioni moja nchini Rwanda. Daktari Eugene Rwamucyo ametiwa mbaroni wakati alipokuwa anashiriki katika maziko ya Jean-Bosco Barayagwiza, ambaye amefia jela wakati alipokuwa anatumikia kifungo kuhusiana na mauaji hayo. Hata hivyo Daktari Eugene amekanusha tuhuma zinazomkabili akidai kuwa, hiyo ni kampeni ya chama tawala nchini Rwanda cha RPF na viongozi wa nchi hiyo ambao amesema wamekuwa wakimsaka tangu miaka 15 iliyopita. Kiswahili Radio |
Thursday, May 27, 2010
Mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari ya Rwanda atiwa mbaroni Ufaransa
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Thursday, May 27, 2010
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
0 comments:
Post a Comment