|
Umoja wa Ulaya
umetangaza kuwa, wakazi milioni 80 wa nchi wanachama wa umoja huo
wanaishi chini ya mstari wa umaskini.
Taarifa ya umoja huo imesema,
kati ya kila watu 7 nchini Ujerumani, mmoja anaishi chini ya mstari wa
umaskini.
Ni kwa sababu hiyo ndio maana umoja huo umeutangaza mwaka
huu wa 2010 kuwa ni Mwaka wa Kupambana na Umaskini na Kutengwa katika
Jamii.
Takwimu zinaonesha kuwa, karibu asilimia 14 ya Wajerumani
wanaishi chini ya mstari wa umaskini.
Miongoni mwa ratiba za umoja
huo za kukabiliana na mgogoro huo ni kujaribu kuongeza kiwango cha elimu
cha wakazi wa nchi wanachama.
Ijapokuwa wataalamu barani Ulaya
wamelipokea vizuri suala la kusaidiwa kifedha Wazungu maskini, lakini
hawaamini kuwa kupandishwa kiwango cha mishahara na kutolewa misaada ya
kifedha na serikali kwa ajili ya watoto, kutasaidia kutatua tatizo hilo
sugu na ndio maana Umoja wa Ulaya unajaribu kutumia mbinu ya kuelimisha
na kutoa mafunzo kama silaha kuu ya kupambana na umaskini huko Ulaya.
|
|
0 comments:
Post a Comment