Na Amina Magona, Ilala
UPANDE wa mashitaka katika kesi
inayowakabili wakurugenzi wanne wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), leo
umeafutia mashitaka yaliyokuwa yakiwakabili vigogo hao na kuwafungulia
mengine mapya.
Kesi hiyo ilikuwa inasikilizwa leo asubuhi mbele ya Hakimu Mkazi, Agnes Mchome.
Wakurugenzi
hao—Simon Jengo ambaye ni Mkurugenzi wa BoT; Naibu Mkurugenzi wa Fedha
za Nje, Kisima Mkango; Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kitengo cha
Sheria; Bosco Kimela na Mkurugenzi wa Huduma za Benki, Ally
Bakari—wanatuhumiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi.
Wakili wa
Serikali, Afrey Sedekia, amedai kuwa washitakiwa hao kati ya mwaka
2004, 2005 na 2007 walitumia madaraka yao vibaya kwa kuchapisha noti
nyingi bila idhini ya Serikali.
Awali washitakiwa hao
ambao mashitaka yao yamefutwa walifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi wa
Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Samwel Maweda na Wakili wa Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ben Lincon, wakikabilia na
makosa ya kuhujumu uchumi na kuisababishia Serikali hasara ya sh.
bilioni 104.
Wakili huyo aliendelea kudai kuwa
washitakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka matatu ambapo shitaka la
kwanza linawahusu Jengo na Mlayo ambao ni washitakiwa wa kwanza na wa
pili.
Katika mashitaka hayo inadaiwa kuwa washitakiwa hao walitumia
nyaraka za Serikali kwa lengo la kudanganya miongozo kinyume cha
kifungu cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa.
Imedaiwa
kuwa washitakiwa hao wawili kwa pamoja mwaka 2004, wakiwa ni waajiriwa
wa Serikali katika BoT ambako walikuwa wakishikilia nyadhifa zao za
sasa waliongeza gharama za usambazaji wa noti ikilinganishwa na gharama
halisi ya mwaka 2001 huku wakijua ni kosa kisheria.
Shitaka la
pili linafanana na la kwanza ambapo linamhusu mshitakiwa wa kwanza,
Jengo, anayedaiwa kutumia nyaraka hizo kumdanganya mwajiri wake ili
aweze kuongeza gharama za uchapishaji wa noti mwaka 2005.
Katika
shitaka la tatu imedaiwa kuwa kati ya mwaka 2004 na 2007 washitakiwa
wote wanne kwa pamoja waliisababishia Serikali hasara ya sh.
104,158,536,146.
Washitakiwa hao wanadaiwa kuwa walitenda kosa hilo wakiwa
waajiriwa wa ofisi ya umma baada ya kushindwa kutimiza wajibu wao kwa
kutobaini maandalizi ya kuandaa mkataba ulioingiwa na BOT, wa
kutengeneza noti mpya uliokuwa na gharama kubwa ikilinganishwa na hali
halisi.
Hata hivyo kesi hiyo imefutwa na kubadilishiwa nyingine leo asubuhi.Kesi hiyo itatajwa tena Mei 21, mwaka huu.
Saturday, May 8, 2010
Vigogo BoT wafutiwa mashitaka
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Saturday, May 08, 2010
Email This
BlogThis!
Share to Twitter
Share to Facebook
0 comments:
Post a Comment