SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, January 25, 2014

VIKUNDI VYA VICOBA VILIVYOPO CHINI YA POVERTY FIGHTING TANZANIA (PFT) INAYOSIMAMIWA NA MBUNGE WA TEMEKE ABBAS MTEMVU VYAKABIDHIWA VIFAA VYA MILIONI 192.3

*NI GARI SITA AINA YA SUZUKI CARRY,  *BAJAJ KUMI, *PIKIPIKI 19 AINA YA BOXER, *PIKIPIKI YA MZIGO AINA YA TOYO, *VIFAA VYA UMEME VYA USEREMALA, *MBAO, *VIFAA VYA STATIORIES NA VIFAA VYA SHOOTING CAMERA
Vifaa vikiwa tayari kukabidhiwa kwa vikundi hivyo vya Vicoba chini ya PFT
 Baadhi ya sare zilizovaliwa na wadau zilikuwa na ujumbe huu
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwezeshaji na Uwekezaji. Dk. Mary Nagu (kushoto) akiwasili ukumbini huku akiwa na Mwenyekiti wa PFT, Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu, kwa ajili ya kuvigawia vifaa mbalimbali  vikundi 130 vya Vikoba vilivyo chini ya Taasisi ya PFT katika hafla iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa PTA, Sabasaba, Dar es Salaam
 Mwenyekiti wa PFT, Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu akimtambulisha kwa waziri Nangu, Mwezeshaji wa VICOBA walioko chini ya PFTJohannes Linde wakati waziri Nagu alipowasili ukumbini.
 Wanavikundi wakilipuka kwa shamrashamra wakati wa mapokezi ya waziri Nagu ukumbini
 Cherekochereko na mabango
 Kina mama wa Vicoba wakifurahi
 Mama Mtemvu na Mwanae wakiwa kwenye hafla hiyo
 Wanachama wa Vicoba wakiwa wamekaa baada ya mapokezi
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Juma Kassim 'Juma Nature' akitumbuiza wakati wa hafla hiyo.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Juma Kassim 'Juma Nature' akitumbuiza kwenye hafla hiyo
 Msanii Snura Mushi maarufu kwa jila na Majanga, akikonga nyoyo za wanavicoba wakati wa hafla hiyo
 Snura Majanga akionyesha umahiri wake mbele ya wana-Vicoba
 Mwenyekiti wa PFT, Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu akimkabidhi Waziri Nagu hati maalum ya shukrani kwenda kwa Rais Jakaya Kikwete kutokana na mchango alioutoa wa sh. milioni 50 kwa PFT. Kushoto ni Naibu Waziri wa Maendeleo na Jamii Jinsia na Watoto Pindi Chana.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji). Dk. Mary Nagu (katikati) akikabidhi pikipiki kwa moja ya vikundi 130 vya Vikoba vilivyo chini ya Taasisi ya PFT katika hafla ya kuviongezea uwezo kwenye Ukumbi wa PTA, Sabasaba, Dar es Salaam leo. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Temeke, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Abbas Mtemvu.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji). Dk. Mary Nagu (katikati) akikabidhi gari kwa moja wa viongozi wa PFT.
Masiriamali ambaye ni mwanachama wa moja ya vikundi cya Vicoba vilivyopo chini ya PFT akiwa kazini wakati wa hafla hiyo
 Wanachama wa Vicoba wakichangamkia fomu za NSSF za Matibabu
 Wanakikundi cha Vicoba wakiwa kwenye gari lao baada ya kukabidhiwa
 Mweneyekiti wa PFT, Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu akizungumza na waandishi wakati wa hafla hiyo
Mtembu akiwa na Kina Juma Nature na Snura Majanga ambao walitumbuiza kwenye hafla hiyo.

 TAARIFA FUPI KWA MHE: WAZIRI WA UWEZESHAJI NA UWEKEZAJI MAMA MARY NAGU KUHUSU POVERTY FIGHTING TANZANIA (PFT) TAREHE 24/01/2014 PTA SABA SABA

Mhe: Mgeni Rasmi Waziri wa Uwezeshaji na uwekezaji Mama Marry Nagu.
Awali ya yote tunachukua fursa hii Kukushukuru kwa kukubali kuwa mgeni rasmi katika shughuli yetu hii muhimu inayowahusu wajasilia mali wa Vicoba wanaoratibiwa na PFT katika Manispaa ya Temeke na tunakukaribisha karibu sana Temeke na ujisikie upo Nyumbani
.
1. UTANGULIZI.
Poverty Fighting Tanzania (PFT) ni Taasisi isiyo ya kiserikali lililosajiriwa chini ya sheria ya mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO) sheria namba 24  kifungu kidogo cha 12 sheria ya mwaka 2002 kwa namba ya usajiri 00NGO/00004071.
Ofisi za PFT zipo Mtaa wa Kitunda Tandika Wilaya ya Temeke,Mkoa wa Dar-es-salaam.
2. Muundo wa PFT:
Mhe: Mgeni Rasmi: PFT inaongozwa na Mkutano mkuu hiki ndio chombo cha juu katika kufanya maamuzi yanayohusina sera,na taratibu za PFT, ikifuatiwa na Bodi ya wakurugenzi  na Menejimenti ambayo inasimamia kazi za siku hadi siku  inayoongozwa na mkurugenzi Mtendaji.
3. Lengo la PFT:
Mh: Mgeni Rasmi:
Lengo la PFT:  Ni kuunganisha Nguvu kazi katika kupambana na Umasikini Tanzania.
Dira ya PFT:  Kujenga jamii ambayo itakuwa huru kutokana na umasikini na maradhi .
Dhamira ya PFT:  Kuleta mabadiliko chanya katika maisha ya jamii kupitia kuanzisha vikundi vilivyoandaliwa na kuwezeshwa kwa ustadi na mitaji ya kutosha.
Mhe: Mgeni rasmi:  Kutokana na malengo hayo PFT inatekeleza shughuli zifuatazo:
·    Kuhamasisha na kuunda vikundi vya Vicoba katika  ngazi chini yaani Grassroots  level
·    Kuwajengea uwezo wanachama wa PFT katika maeneo makuu matatu:
i.    Mfumo wa Vicoba namna unavyofanya kazi
ii.    Stadi za uongozi wa vikundi na ujasilia mali
iii.    Kuwaunganisha wanachama wa Vicoba wa PFT na wadau wengine wa maendeleo  kwa lengo la kujenga ubia na kubadilishana uzoefu,taarifa, maarifa na kupanua masoko yao.
4. Walengwa wa mradi:
Mhe: Mgeni Rasmi:
Katika kutekeleza program ya kupunguza umasikini ,walengwa wa mradi huu ni familia zenye kipato cha chini ,jamii iliyoko pembezoni mwa huduma za kifedha na makundi maalumu.
5. Mafanikio  ya mradi huu:
Mhe: Mgeni rasmi: Hadi kufikia sasa PFT imefanikiwa  kuunda jumla ya Vikundi 130 venye wanachama 2,228 wanawake wakiwa 1,956 sawa na asilimia 87.8 na wanaume wakiwa 272 sawa na asilimia 12.2  wanachama hao wamewekeza jumla ya Tshs: 833,967,140 kupitia mpango wa ununuzi wa hisa za kila wiki na kuchangia mfuko wao wa jamii, fedha zote hizo zinamilikiwa na wanakikundi wenyewe kupitia akaunti  zao 105 zilizofunguliwa Amana Benki  zinazotumika kuifadhi fedha za  mizunguko yao na marejesho ya mikopo yao wanayokopeshana.
Jumla ya mikopo 1,240 yenye thamani ya Tshs: 584,729,000 imetolewa na wana vikundi wenyewe kupitia mifuko yao ya hisa.
Mhe: Mgeni Rasmi  Jumla ya Tshs: 75,779,900 zimegawiwa kwa wanachama hao ikiwa faida itokanayo na mikopo wanayokopeshana kwa kipindi cha miaka 3 sasa.
Mhe: Mgeni Rasmi  pia tumefanikiwa  kuwaunganisha wanachama wa PFT na Taasisi ya kifedha yaani Amana Benki ambayo imekubali kuwakopesha wanachama hao kupitia  PFT jumla ya Tshs: 300,000,000 kwa kuthaminisha bidhaa wanazohitaji wanachama wa PFT ili waweze kukuza shughuli zao za kiuchumi, miongoni mwa mikopo hiyo ndiyo hii ambayo leo utakabidhi  gari aina ya Suzuki carry  6 ,Bajaj 10, Pikipiki aina ya Boxer 19, toyo la kubebea mizigo 1, vifaa vya selemala  vinavyotumia umeme, mbao,vifaa vya  statiories  na vifaa vya shooting Camera kwa vikundi 19 vinavyoratibiwa na PFT vyote vikiwa na thamani ya Tshs: 192,321,000/=
6. Changamoto
Mhe Mgeni Rasmi :
Pamoja na mafanikio yote hayo bado PFT inakabiliwa na changamoto nyingi katika kutimiza malengo yake baadha ya changamoto hizo ni:
i.    Ugumu wa upatikanaji wa mikopo ya masharti nafuu, kwani hata huu mkopo tuliyopata amana tumechukua muda mrefu zaidi ya 5 na Dhamana kubwa iliyowekwa ndio tumefanikiwa kupata mkopo huo kwaiyo hiyo changamoto inayowasumbua wajasilia mali wengi wadogo Tanzania.
ii.    Upungufu wa fursa za kupata elimu ya ujasilia mali zaidi kwa wanachama wetu na kujenga ubia  na wadau wengine wa ndani na je ya nchi kupitia wizara ya uwezeshaji na uwekezaji .
7. Hitimisho:
Mhe:  Mgeni Rasmi :
Mwisho tunaludia tena kukushukuru wewe binafsi na msafara wako mliongozana nao kuja katika shughuli hii  muhimu kwa wajasilia mali wa Temeke, PFT ina imani kubwa na wewe.
Mhe: Mgeni Rasmi : Sisi tunakujua kuwa  una moyo na upendo  kwa PFT na  hiyo imedhirika tena kwa mara ya pili leo,kwani mara ya kwanza Tulikutana ofisini kwako Dodoma mwezi February 2013  ulikuwa na majukumu mengi na msarafa wetu ulikuwa wa ghafla sana  lakini ulitupokea na kutusaidia kwa kutuunganisha na Viongozi wa Baraza la uwezeshaji la Taifa ahsante Mhe: Waziri.

Mhe: Mgeni Rasmi: kupitia kwako Menejimenti , Bodi ya Wakurugenzi  na wanachama wote wa PFT  tunampongeza sana mwenyekiti wetu wa bodi Mhe; Abbas  Mtemvu ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Temeke kwa usimamizi wake makini wa PFT hadi kufikia mafanikio haya.
Imani yetu ni kwamba utaendelea kushirikiana nasi na  kutusaidia mara kwa mara kwa kadri ya uwezo wako  ili wajasilia mali hawa wa Temeke waweze kufaidika na fursa zinazotokea katika wizara yako ambazo zinawalenga wao.
Tunakutakia kila heri na mafanikio katika utendaji wako wa majukumu ya kitaifa,Sisi PFT tutaendelea kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha tunatekeleza mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umasikini wa kipato Tanzania (MKUKUTA II)
Karibu tena Temeke wewe na msarafa wako
Naomba kuwasilisha:
VICOBA SILAHA DHIDI YA UMASIKINI
NI MARUFUKU KUKATA TAMAA

0 comments:

Post a Comment