SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, May 8, 2010

Maskini watoto hawa

JESHI la Polisi Mkoa wa Ruvuma linamshikilia mwanamke Asha Salum kwa tuhuma za kuwacharanga mapanga watoto wake wanne kwa madai kuwa wameiba wali.
Mtuhumiwa huyo inadaiwa kuwa alipika chakula hicho kisha yeye kuondoka na kwenda kilabu kunywa pombe.
Imedaiwa kuwa baada ya kurejea nyumbani ndipo alipobaini kuwa chakula hicho kimeliwa na watoto wake, jambo ambalo lilimkera na kuamua kuwafungia chumbani kisha kuanza kuwacharanga kwa panga.
Kutokana na hali hiyo, watoto hao walipiga mayowe ya kuomba msaada ambapo majirani wakijitokeza kisha kutoa taarifa polisi na kuwakimbiza watoto hao hospitali kwa ajili ya matibabu zaidi.
Hata hivyo, mama huyo alikiri kutenda kosa hilo baada ya kunaswa na Polisi kisha kudai kuwa alipitiwa na shetani.
Majeruhi hao wamelazwa hospitali ya Mkoa wa Songea wakiendelea kupatiwa matibabu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Michael Kamuhanda, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mtuhumiwa anashikiwa na atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

0 comments:

Post a Comment