LILONGWE
Mahakama nchini Malawi leo imewahukumu mashoga wawili wa
kiume kifungo cha miaka 14 gerezani, baada ya kupatikana na hatia
ya kulawiti na kufanya vitendo kinyume na maadili.
Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Nyakwawa Uisiwausiwa amesema ametoa adhabu hiyo kali kwa sababu anataka kuwazuia watoto wa kike na kiume wa Malawi wasijiingize katika ndoa za jinsia moja.
Hakimu huyo amesema kuwa ndoa za aina hiyo ni kosa kwa kuwa haziendani na utamaduni wa Malawi wala imani za kidini. Mashoga hao, Steven Monjeza, mwenye umri wa miaka 26 na Tiwonge Chimbalanga, mwenye umri wa miaka 20 walikamatwa baada ya kufunga ndoa mwezi Desemba, mwaka uliopita.
Mnamo siku ya Jumanne shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu la Amnesty International lilitoa wito wa kuachiwa haraka kwa mashoga hao. Shirika hilo limesema kushikiliwa kwa mashoga hao ni kukiuka haki zao za kibinaadamu.
Deusche Welle.

0 comments:
Post a Comment