Msemaji wa Umoja wa Mataifa ametangaza kuwa, umoja huo utatuma maafisa wake wawili wa ngazi za juu nchini Sudan kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais Omar al Bashir wa nchi hiyo.
Marie Okabe amesema kwamba, Haile Menkerios Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa Sudan na Ibrahim Gambari Mkuu wa Mpango wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika huko Darfur watahudhuria sherehe hizo zitakazofanyika tarehe 27 mwezi huu wa Mei.
Rais Omar al Bashir wa Sudan mwezi uliopita alichaguliwa kwa kura nyingi katika uchaguzi mkuu, na hivyo kumuwezesha kuiongoza tena nchi hiyo.
0 comments:
Post a Comment