Mamia ya
wananchi wa Niger wengi wao wakiwa wanawake na watoto wadogo
wamekimbilia nchi jirani ya Nigeria kutafuta chakula. Sani Makana,
Kamishna wa Kilimo wa jimbo la Katsina Nigeria, amesema kuwa, serikali
ya nchi hiyo inajua kwamba raia wengi wa Niger wamekimbilia katika
baadhi ya maeneno ya kusini mwa jimbo hilo.
Ameongeza kwamba, baadhi yao wana hali mbaya sana kiasi kwamba wamelazimika kuomba-omba milangoni mwa nyumba za watu. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, karibu watu milioni 7.8 nchini Niger wanahitajia msaada wa chakula. Serikali ya mpito ya Niger mwishoni mwa wiki ilitangaza kuanza operesheni ya kugawa chakula kwa karibu watu milioni 1.5 wanaokabiliwa na njaa nchini humo. Mawaziri wa nchi za Afrika Magharibi pia, siku ya Jumatano walikutana

katika mji mkuu wa Togo, Lome kujadili matatizo ya chakula katika nchi
hizo.
0 comments:
Post a Comment