SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, May 22, 2010

Ndege ya abiria ya India yaanguka na kusababisha vifo vya watu 158


Vyombo vya habari vya India tarehe 22 vimeripoti kuwa, ndege aina ya Boeing 747 ya kampuni ya ndege ya India siku hiyo asubuhi ilianguka huko kusini mwa India. Jumla ya idadi ya abiria na wafanyakazi waliokuwemo kwenye ndege hiyo ni 166, ambapo watu 158 wamefariki, na wengine wanne wamenusurika.
Ofisi ya kampuni ya ndege ya India huko Dubai tarehe 22 ilithibitisha kuwa, abiria waliokuwemo kwenye ndege hiyo wote ni kutoka India.
Kabla ya kuanguka, ndege hiyo haikutoa ombi la uokozi. Marubani wote wawili walioendesha ndege hiyo si wahindi. Mmoja kati yao anatoka Russia. Baada ya ndege hiyo kuanguka, idara za polisi na zima moto za huko zilifanya uokoaji mara moja.
Waziri mkuu wa India Bw. Manmohan Singh alitoa salamu za rambirambi kutokana na watu waliokufa kwenye ajali hiyo, na kutoa salamu za pole kwa familia za watu waliokufa, pia alitoa amri ya kuilipa kila familia ya watu waliokufa Rupia laki mbili.
Mpaka sasa, chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana na uchunguzi unaendelea.
Kiswahili Radio

0 comments:

Post a Comment