SEOUL
Korea Kaskazini imesema itakata uhusiano wake na Korea Kusini mpaka rais wa nchi hiyo Lee Myung-bak atakapoondoka madarakani mnamo mwaka 2013. Korea Kaskazini imechukua uamuzi huo kufuatia hatua ya Korea Kusini kuilaumu kwamba iliishambulia na kuizamisha meli yake ya kivita mnamo mwezi Machi mwaka huu ambapo mabaharia 46 wa Korea Kusini waliuwawa.
Kwa mara nyengine tena hapo jana Korea Kaskazini ilikanusha madai hayo. Korea Kaskazini pia imetangaza kwamba inawandaa wanajeshi wake kwa vita.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema uamuzi wa Korea Kaskazini kusitisha kabisa uhusiano na jirani yake Korea Kusini ni uchokozi wa hali ya juu katika rasi ya Korea.
Kusambaratika kwa uhusiano kati ya Korea Kaskazini na Korea Kusini kunatokea huku waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani Hillary Clinton akitarajiwa kuwasili mjini Seoul hii leo kwa mazungumzo.
Deutsche Welle.

0 comments:
Post a Comment