Mwakilishi wa China katika ofisi
ya Umoja wa Mataifa huko Geneva Balozi He Yafei tarehe 25 alihudhuria
Baraza la 2 la Afrika kwa Mazungumzo (African Forum for Dialogue)
lililofanyika huko Geneva.
Balozi huyu alizumgumzia uhusiano wa kimkakati na kiwenzi kati ya Afrika na China akisema:
"China ni nchi kubwa zaidi inayoendelea, na Afrika ni bara lenye nchi nyingi zaidi zinazoendelea, na ushirikiano kati ya China na Afrika ni sehemu muhimu ya ushirikiano ya kusini na kusini. Kuimarisha urafiki na ushirikiano kati yake na Afrika, na kuunga mkono amani na maendeleo ya Afrika ni sera ambayo China inafuata kithabiti."
Baraza la Afrika kwa Mazungumzo lilianzishwa mwaka 2009 huko Geneva na mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Jean Ping. Kauli mbiu ya baraza la mwaka huu ni "Amani na Maendeleo ya Afrika Yasukuma Mbele Maendeleo Endelevu". Watu wapatao 300 walishiriki kwenye baraza hilo, wakiwa ni pamoja na wajumbe kutoka nchi za Afrika, Shirika la Mkutano wa Biashara na Maendeleo la Umoja wa Mataifa, na wawakilishi wa China, Marekani, Japan, Russia na nchi nyingine katika ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Geneva.
swahili.cri.cn.

0 comments:
Post a Comment