Saturday, May 22, 2010
Jela miaka 30 kwa kubaka shemejiye
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi mjini Singida imemfunga miaka 30 jela mkazi wa kijiji cha Minyenye, Saidi Msasu (25), baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mke wa kaka yake.
Ilidaiwa na Mwendesha Mashitaka Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Majaliwa Ntilimbuza, mbele ya Hakimu Chiganga Tengwa kuwa Julai 17, mwaka juzi katika kijiji cha Minyenye, mshitakiwa Msasu alimwingilia kwa nguvu shemeji yake (jina linahifadhiwa) na kumsababishia maumivu makali sehemu za siri.
Ntilimbuza alidai kuwa siku ya tukio mshitakiwa alikwenda nyumbani kwa kaka yake, Abeid Labia na kumkuta shemeji yake amejipumzisha nje ya nyumba.
Alijulishwa kuwa kaka yake hayupo, ghafla alimrukia shemeji yake kwa nguvu na kumkokota hadi ndani ya nyumba yao.
Majaliwa alidai baada ya kumwingiza ndani ya nyumba, alimwangusha na kumkaba koo, kitendo kilichofanya asiweze kupiga kelele.
Alisema, baada ya kumwangusha chini, alimchania nguo ya ndani na kumbaka. Wakati akiendelea, mshitakiwa aliishiwa nguvu hatua iliyomsaidia mlalamikaji kuondoa mkono kooni na kupiga mayowe.
Majaliwa alidai mume wa mlalamikaji alifika mara moja kwenye tukio na kumkuta mdogo wake akiwa amemwangusha chini mkewe huku akiendelea kumbaka.
Mwendesha Mashitaka alidai kuwa baada ya kushuhudia kitendo hicho kwa macho yake, alipiga mayowe na ndugu zake waliokuwa karibu walifika.
Hata hivyo, ilidaiwa kuwa mshitakiwa aliwaponyoka na kukimbia, lakini alipofika kijiji jirani cha Ikiwu aliishiwa nguvu na kujificha ndani ya nyumba ya mtu asiyemfahamu na kujifungia,kundi la watu lilivunja mlango na kumtoa nje.
Hakimu Tengwa amesema,ushahidi wa upande wa mashitaka umethibitisha bila shaka, kuwa mshitakiwa ana hatia.
Mshitakiwa aliiomba mahakama umwonee huruma na kumpa adhabu ndogo kwa vile hilo lilikuwa kosa la kwanza.
Imeandikwa na Abby Mkungu
HabariLeo.
"Mahakama imezingatia utetezi wako, lakini kutokana na uzito wa kosa ninakupa adhabu ya kutumikia jela kifungo cha miaka 30 ili liwe fundisho kwako na kwa watu wengine wanaokusudia kufanya makosa ya aina hii,"
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Saturday, May 22, 2010
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
0 comments:
Post a Comment