
wapiganaji wa AL shabaab
Vikosi vya serikali Somalia
vimefanikiwa kuidhibiti upya ikulu ya rais katika mji mkuu Mogadishu
baada ya hapo awali wapiganaji wa kiislamu kuishambulia.
Maafisa wanasema washambuliaji wapatao watano kutoka kundi la al-Shabab - waliuawa walipoingia katika eneo la ikulu hiyo.Washambuliaji hao wanadaiwa kulipua bomu lililotegwa kwenye gari karibu na langu kuu la Ikulu hiyo.



