Wakazi wa jiji
la Dar es Salaam na vitongoji vyake kesho wanatapa fursa ya kulitumia
kwa mara ya kwanza Daraja la Kigamboni linalotarijiwa kufunguliwa rasmi
na Rais John Pombe Magufuli siku ya Jumanne ya wiki ijayo ili ‘kuonja’
na kujionea ubora wa daraja hilo kisasa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Meneja mradi kutoka kampuni ya China
Railway Construction Engineering Group ambao wametekeleza mradi huo kwa
ushirikiano na kampuni ya China Railway Major Bridge Group Bw. Zhang Bangxu, alisema siku ya kesho, wataruhusu wakazi hao na magari kupita katika daraja hilolililogarimu Dola za Kimarekani milioni 135 kujengwa.
“Kama wajenzi kesho tutaruhusu
magari kupita kwenda upande wa Kurasini na upande wa Kigamboni siku ya
Jumamosi tu kama ikiwa ni sehemu ya majaribio yetu kitaalamu ikiwa ni
pamoja na kutumia fursa hiyo kufanya majaribio ya mitambo na mashine
zote ambazo zitatumika katika kufanya tozo mbali mbali baada ya kuanza
rasmi kwa mradi,” alifafanua
Kwa mujibu wa Bw. Bangxu,
daraja la Kigamboni ndiyo daraja refu kuliko yote katika ukanda wa
Afrika Mashariki lililotengenezwa kwa kutumia teknolojia ya matumizi ya
kamba (cable) kubeba uzito wa daraja, ambayo itaunganisha jiji la
kibiashara la Dar es Salaam na eneo la Kigamboni na Kurasini. Ujenzi
ulianza mnamo Tarehe moja Februari mwaka 2012.
“Pamoja na kujengwa katika ubora
wa hali ya juu, daraja hili lina jumla ya njia sita yaani njia tatu kwa
kila upande, pamoja na njia mahususi kwa ajili ya waenda kwa miguu na
waendesha baiskeli ambayo ina upana wa mita 2 na nusu (2.5 meters)
katika kila pande. Daraja hilo litaruhusu magari yenye uzito usiozidi
tani 30 kupita.,’’ aliongeza
Bw. Bangxu alisema
kwamba kaskazini mwa daraja hilo, litaungana na barabara lenye urefu wa
kilometa moja ambayo inakatiza reli ya TAZARA kisha kuungana na
barabara ya Mandela. Kwa upande wa Kigamboni, daraja litaungana na
barabara lenye urefu wa Kilometa 1.5 ambayo inaungana na barabara ya
Kigamboni Ferry – Kibada.
Aliongeza kwamba kukamilika kwa
daraja hili ni ishara ya maendeleo kwani inatarajiwa kuchochea kasi ya
maendeleo ya mji wa kisasa wa Kigamboni (Kigambani satellite city),
kutengeneza fursa za ajira katika sekta ya ujenzi wa maeneo ya makazi
pamoja na sekta za huduma ambazo zitastahimili ongezeko kubwa wa idadi
ya wakazi wapya katika mji huo mpya.
Kukamilika kwa daraja hilo
kunatajwa kuwa kutawapafusra wakazi wa Kigamboni na viunga vyake ikiwa
ni kutoa njia mbadala ya kufikia makazi yao, biashara zao au shuguli zao
za ujenzi wa taifa kwa njia ya barabara.
Maeneo ya Kigamboni na Kurasini
kwa sasa hufikika kwa kutumia vivuko viwili vya MV Magogoni na MV
Kigamboni ambazo kwa pamoja zinaumezo wa kubebe abiria 1000 na magari 78
kwa kila safari.
Mradi huo umedhaminiwa kwa kwa
ubia kati ya Shirika la Hifadhi ya Jamii ya Taifa (NSSF) na Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
0 comments:
Post a Comment