Mkuu
wa ofisi na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira
Rodrigues akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki (Utawala na Fedha), Bw. Liberat Mfumukeko alipowasili katika
chumba maalum cha wageni kabla ya kuelekea kwenye ufunguzi wa kongamano
la siku tatu la Mtandao wa Redio za Jamii katika nchi za Afrika
Mashariki (EACOMNET) linalolenga kujadili namna ya kuziwezesha redio
hizo kujiendesha katika mipango endelevu kwa kuwa na mipango sahihi ya
kifedha bila kutegemea fedha kutoka kwa wafadhili ili ziweze kutoa
mchango unaokusudiwa kwa wananchi linaloendelea katika makao makuu ya
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) jijini Arusha.(Picha zote na Modewjiblog)
Na Modewjiblog Team, Arusha
SHIRIKA
la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni
(UNESCO), limeonyesha nia yake ya kuendeleza utamaduni wa kuzisaidia
redio za jamii nchini Tanzania kwa lengo la kuwawezesha Watanzania walio
wengi kupata elimu na hatimae kujinasua katika umaskini.
Akizungumza
katika ufunguzi wa kongamano la Mtandao wa Redio za Jamii katika nchi
za Afrika Mashariki (EACOMNET) linalofanyika makao makuu ya Jumuiya ya
Afrika Mashariki(EAC) mjini Arusha, Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi mkazi wa
UNESCO Zulmira Rodrigues alisema kwamba watu zaidi ya milioni 16 wengi
wao wakiwa pembezoni mwa Tanzania wanategemea redio za jamii katika
kuelimishwa masuala mbalimbali ya ustawi wa jamii jambo ambalo shirika
lake linawajibika kwa redio hizo kwa kutoa misaada mbalimbali ili ziweze
kujitegemea na kutoa huduma zake kikamilifu.
Alisema
anaamini kwamba kwa miaka kadhaa ijayo redio za jamii zitakuwa chanzo
cha maarifa kwa watu wengi nchini Tanzania kutokana na uasilia wake na
kwa kuyatumikia maeneo ambayo kimawasiliano ni vigumu kufikika, na
wakati huo huo vyombo vikuu vya mawasiliano kushindwa kukidhi mahitaji
ya wanajamii jambo linalosababisha ukosefu wa kupata habari muhimu na
kuzorotesha maendeleo katika jamii husika.
Naibu
Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (Utawala na Fedha), Bw.
Liberat Mfumukeko akisalimiana na Mwenyekiti wa Radio za Jamii kutoka
UNESCO India, Prof. Vinod Pavarala katika chumba maalum cha
wageni katika makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) jijini
Arusha.
Zulmira
amezihimiza redio hizo kutoa huduma zinazostahili kwa jamii za kupasha,
kuelimisha na kuburudisha, pamoja na kujiwekea mikakati wa kudumu ya
kuhamasisha rasilimali fedha zitakazosaidia kuboresha huduma za redio na
kuboresha mfumo wa mawasiliano kati kituo cha redio na wanajamii.
Miongoni
mwa maboresho yatakayoendelezwa na Unesco ni kusaidia uhakiki wa ubora
wa matangazo, vipindi vyenye kuzingatia maadili na ushirikishwaji wa
makundi yote wakiwemo wanawake ,vijana ,watu wenye ulemavu na Albinism
katika mchakato wa demokrasia, amani na maendeleo .
Kongamano
hilo la siku tatu pamoja na mambo mengine linalenga kujadili namna ya
kuziwezesha redio hizo kujiendesha katika mipango endelevu kwa kuwa na
mipango sahihi ya kifedha bila kutegemea misaada kutoka kwa wafadhili
ili ziweze kutoa mchango unaokusudiwa kwa wananchi.
Kwa
niaba ya mtandao wa redio jamii ukanda wa Afrika Mashariki, mwenyekiti
wa Mtandao wa redio za Jamii Tanzania, COMNETA Joseph Sekiku
aliishukuru Unesco kwa kuziwezesha redio za jamii kutoka nchi za Afrika
Mashariki kukutana kwa lengo kushirikiana na kupeana maarifa kuhusu
uendeshaji wa redio hizo na zitakavyoweza kutekeleza kwa ubora malengo
17 ya dunia ya maendeleo endelevu na UNESCO India kwa kuleta maarifa
mapya kuhusu uendeshaji wa redio za jamii.
Mkuu
wa Ofisi na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira
Rodrigues (kulia) akibadilishana mawazo na Naibu Katibu Mkuu mpya wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki (Utawala na Fedha), Bw. Liberat Mfumukeko
katika chumba maalum cha wageni kabla ya kuelekea kwenye ufunguzi wa
kongamano la siku tatu la Mtandao wa Redio za Jamii katika nchi za
Afrika Mashariki (EACOMNET) linalofanyika makao makuu ya Jumuiya ya
Afrika Mashariki (EAC) jijini Arusha.
Nchi
zilizoshiriki katika kongamano hilo ni Burundi, Kenya, Rwanda na Uganda
chini ya mwamvuli wa Mtandao wa Redio za jamii Afrika mashariki
(EACOMNET), ukiwa na redio wanachama 50 zenye uwezo wa kuwafikia
wasikilizaji milioni 35 kati ya watu milioni 120 waliomo katika nchi
hizo.
Naibu
Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (Utawala na Fedha),
Liberat Mfumukeko ameelezea kufurahishwa kwake kufanyika kwa kongamano
hilo ambalo litasaidia redio jamii kupata maarifa zaidi na elimu kuhusu
mtengamano wa Afrika Mashariki na kuufanikisha.
Alisema
Jumuiya ya Afrika Mashariki inaelewa umuhimu wa vyombo vya habari hasa
vya jamii kutokana na kazi yake kwa kuzingatia juhudi utekelezaji wake
wa kuhamasisha jamii kuendeleza mtengamano wa Afrika Mashariki.
Mwenyekiti
wa Mtandao wa redio za Jamii Tanzania, (COMNETA), Joseph Sekiku
akizungumza kwa niaba ya mtandao wa redio jamii ukanda wa Afrika
Mashariki (EACOMNET) kabla ya kumkaribisha Prof. Vinod Pavarala.
Mwenyekiti
wa Radio za Jamii kutoka UNESCO India, Prof. Vinod Pavarala akieleza
dhumuni na lengo la kongamano hilo kwa washiriki. Kulia ni Mkuu wa Ofisi
na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la UNESCO nchini, Zulmira Rodrigues.
Mkuu
wa Ofisi na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira
Rodrigues akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Katibu
Mkuu mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (Utawala na Fedha), Bw. Liberat
Mfumukeko kufungua rasmi kongamano hilo linaloendelea jijini Arusha.
Naibu
Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (Utawala na Fedha), Bw.
Liberat Mfumukeko akifungua rasmi kongamano la siku tatu la Mtandao wa
Redio za Jamii katika nchi za Afrika Mashariki (EACOMNET) linalolenga
kujadili namna ya kuziwezesha redio hizo kujiendesha katika mipango
endelevu kwa kuwa na mipango sahihi ya kifedha bila kutegemea fedha
kutoka kwa wafadhili ili ziweze kutoa mchango unaokusudiwa kwa wananchi
linaloendelea katika makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)
jijini Arusha.
Mwenyekiti
wa Radio za Jamii kutoka UNESCO, Prof. Vinod Pavarala akimkabidhi Ofisa
Miradi katika kitengo cha Mawasiliano, Habari na Tehama UNESCO, Bw. Al
Amin Yusuph zawadi kwa heshima ya ukumbusho wa India.
Ofisa
Miradi katika kitengo cha Mawasiliano, Habari na Tehama UNESCO, Bw. Al
Amin Yusuph akitoa shukrani zake kwa Prof. Vinod baada ya kupokea
zawadi.
Ofisa
miradi mpya katika kitengo cha Mawasiliano na Tehama UNESCO, Nancy
Kaizilege akijitambulisha kwa hadhira ya washiriki wa kongamano.
Sehemu ya washiriki katika kongamano hilo.
Mhadhiri
wa Chuo cha Uandishi wa Habari cha Hyderabad India, Dkt. Kanchan Malik
akiongoza kikundi kazi kilichojumuisha washiriki kutoka Rwanda na
Uganda.
Mwenyekiti
vyombo vya Habari Jamii kutoka UNESCO India, Prof. Vinod (aliyeipa
mgongo camera) akiongoza kikundi kazi kinachojumuisha washiriki kutoka
Burundi na Tanzania.
Mkuu
wa Ofisi na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira
Rodrigues akifurahi jambo na Mjumbe wa bodi udhamini ya Mtandao wa Radio
Jamii Tanzania (COMNETA), Balozi Mstaafu, Christopher Liundi nje ya
chumba cha mikutano makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)
jijini Arusha.
Mjumbe
wa bodi udhamini ya Mtandao wa Radio Jamii Tanzania (COMNETA), Balozi
Mstaafu, Christopher Liundi (kushoto) akibadilishana mawazo na Naibu
Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (Utawala na Fedha), Bw.
Liberat Mfumukeko wakati wakielekea kwenye zoezi la picha ya pamoja.
Picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa kongamano hilo.
Mkuu
wa ofisi na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira
Rodrigues akiwapungia kama ishara ya kuagana na washiriki wa kongamano
hilo wakati akiondoka makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)
jijini Arusha kuanza safari ya kuelekea uwanja wa ndege tayari kurejea
Dar es Salaam.
--
0 comments:
Post a Comment