Suneeta Reddy, mkurugenzi wa hospitali za Apollo
Na Mwandishi Wetu,
Saratani
inasemwa kuwa chanzo kikubwa cha pili kinachosababisha vifo ulimwenguni.
Saratani ya matiti peke yake inaripotiwa kuwa ya pili kama sababu kubwa
ya vifo vinavyohusisha saratani kwa wanawake nchini Tanzania. Kuchelewa
kupata ugunduzi wa haraka na tiba kwa wagonjwa wengi wa saratani ya
matiti kunachangia kuleta ugumu kwenye matibabu pale ugonjwa unapoingia
ngazi ya juu zaidi. Gonjwa hili limeendelea kuwa janga hasa kwa nchi
zinazoendelea.
Ulimwenguni,mwezi
Oktoba ni mwezi maalumu wa kutoa maarifa na elimu juu ya saratani ya
matiti. Kwa kawaida tarehe 19 Oktobanikilele cha saratani ya matiti
nalengo kuu likiwa ni kutoa maarifa ya msingi na yenye faida kuhusiana
na ugonjwa huo. Silaha bora ya kupigana na saratani ya matiti ni
kuigundua mapema.
Ongezeko
kubwa la namba ya vifo kutokana na saratani linatikisa Tanzania, jinsii
navyoathiri namba kubwa ya wanawake kwa sasa. Kutokana na takwimu za
hivi karibuni kutoka hospitali ya Ocean Road kitengo cha saratani
(ORCI), tafiti zinaonyesha ongezeko kubwa la namba kutoka mwaka
2013-2014 (nusu ya kwanza ya mwaka) zaidi ya kesi mpya 400
zimeripotiwa.
Maoni
kwenye hizo takwimu, Dk. Crispin Kahesa mkurugenzi wa Ocean National
Health Insurance Fund alisema kutokana na wingi wa vifo vitokanavyo na
saratani, lazima kuwe najitihada shirikishi zakupigana na saratani ya
matiti.
Kuhamasisha
njia bora za afya kwenye matukio kama haya imekuwa ni wajibu mkuu kwa
hospitali za Apollo ambazo zimetunukiwa tuzo za kimataifa.
Katika
kuhamasisha na kutoa elimu kuhusu maada hii, mkurugenzi wa hospitali za
Apollo, Suneeta Reddy, amesema kwa miaka sasa,saratani ya matiti
imedhihirika kuwa moja ya janga kubwa kwa wanawake wote ulimwenguni. Ni
muhimu kwa wanawake wote kujali afya zao maana wanamajukumu makubwa sio
tu kwenye familia ila pia kwenye jamii kwa ujumla. Wajibu wa mwanamke
mara zote haupo tumuhimu kwenye maisha ya familia ila pia kwenye nyanja
za jamii na uchumi hasa kwa nchi zinazoendelea.
Ukosefu
wa elimu na hamasa umesababisha wimbi kubwa la wanawake kukosa fursa ya
kugundua mengi kuhusu saratani ya matiti. Njia pekee ya kufanya hayo ni
kupata elimu sahihi na uelewa wa kina kuhusu nini ni saratani ya
matiti.
Elimu yakutosha inatakiwa itolewe kwa jamii kusaidia kupunguza zigo la ugonjwa huu. Saratani ya matiti kama isipogundulika mapema itapelekea kifo moja moja. Alisema Suneeta Reddy, mkurugenzi wa hospitaliza Apollo.
Elimu yakutosha inatakiwa itolewe kwa jamii kusaidia kupunguza zigo la ugonjwa huu. Saratani ya matiti kama isipogundulika mapema itapelekea kifo moja moja. Alisema Suneeta Reddy, mkurugenzi wa hospitaliza Apollo.
Hebu
tuanze kufanya kitu sasa hivi. Chagua njia ya ugunduzi, jifanyie
uchunguzi mwenyewe wa saratani ya matiti au kwa kutumia kifaa
kijulikanacho kitaalamu kama mammogram hiki ni chombo madhubuti
kitakacho saidia kugundua ugonjwa katika ngazi ya awali kabisa, alisema
mkurugenzi Suneeta Reddy.
Ugunduzi
wa saratani ya matiti mapema kwa kutumia kifaa cha mammography
kumepunguza vifo vingi kwa wanawake ambao walionekana hawana dalili
zozote waliokuwa na uvimbe na waliokuwa hawana uvimbe kwaile ngazi ya
kwanza.
Mkg.SuneetaReddy anawataka watanzania wote tuheshimu na tutenge dakika tano tu za kujifanyia uchunguzi, alisema.
Kwa
kushirikiana na wito wa Mkg. Suneeta Reddy kuhusu ugunduzi wa saratani
ya matiti katika ngazi ya awali, mkuu wa idara ya mionzi katika
taasisiya Ocean Road, Dk. Yekebeth Vuhahula, aliongeza kuwa saratani ya
matiti bado ni changamoto kubwa Tanzania kwasababu wanawake wengi
wanashindwa kujitokeza mapema kwa matibabu. Kwa jinsi ambavyo saratani
ya matiti inazidi kukomaa na kusambaa, ndivyo inasababisha nafasi ndogo
ya matitabu kufanya kazi. Kama saratani ya matiti ikigundulika mapema
inatibika kirahisi.
Kwa ujuzi
wake kuhusu wagonjwa wa saratani ya matiti Tanzania, wanawake wa
Tanzania wanaoufahamu mdogo na wengine hawana ufahamu kabisa kuhusiana
na vitu hatarishi, dalili, na matibabu ya saratani ya matiti. Imani
potofu kutoka kwenye jamii na tamaduni ni sababu nyingine zinazopelekea
saratani ya matiti kuwa sugu kwa wanawake hapa nchini.
Kuhusu Hospitaliya Apollo
Hospitaliza
Apollo ni za kwanza katika eneo la Asia Pacific kutoa huduma za
upasuaji kwa kutumia mfumo huu wa Robot, ambayo ni aina ya upasuaji
isiyo kuwa na madhara. Taasisi ya upasuaji kutumia Robot iliyopo
hospitalini hapo wamejitoa kipekee katika kutoa huduma bora kwa
wagonjwa.
Taasisi
inawataalamu waliobobea kwenye mafunzo ya upasuaji, upendo katika
utoaji wa huduma vifaa vya matibabu vya kisasa vinavyolenga kutoa uzoefu
bora kwa mgonjwa. Vifaa hivyo ni pamoja na vifaa Robot ya Da Vinci
inayotumika katika upasuaji.
Mfumo
huu wa upasuaji hutumika katika teknolojia ya upasuaji wa magonjwa
yanayohusiana na mfumo wa mkojo (Urology), magonjwa ya wanawake
(Gynaecology), moyo, utumbo, na magonjwa ya watoto na matatizo ya uti wa
mgongo.
0 comments:
Post a Comment