SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, June 23, 2015

Soma Ushuhuda huu toka kwa Mwanachuo Wilbard Patrice utakugusa kwa namna ya kipekee, Hususani ikiwa Mwajiriwa au ni Mwanafunzi kama yeye!

PENYE NIA PANA NJIA:
Anaitwa Wilbard Patrice Mallya ni mzaliwa wa Kwanza katika Familia ya Mr. Patrice Mallya wa mjini Arusha, na kwa sasa anaishi Dar Es Salaam!!
Akiwa kama Mwanafunzi katika Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam, Shahada ya Mahusiano kwa Uma na Utangazaji Yani (B.A in Public Relation and Advertising)

Lakini vilevile pia ni Network Marketing Professional, akiwa kama Mmiliki wa Biashara ya Forever Living, yani Forever Business Owner (FBO)

Akiwa kama Kijana kabla hajajiunga na chuo kikuu wakati bado akiwa kidato cha sita, alikuwa akitamani sana kuishi maisha ambayo wanaishi watoto wa ndugu zake wenye mafanikio, Akiwa ametokea kwenye Familia ya Kawaida sana, Mama akiwa Mwajiriwa na Baba akiwa mfanya biashara wa kawaida, hakuweza kupata nafasi ya kuishi Maisha ya Kifahari kama wenzake, na hivyo basi alikuwa akimwomba sana Mungu afaulu Vizuri Mitiani yake ya mwisho ili achaguliwe kujiunga na chuo kikuu. Na mwenyezi Mungu alimsaidia hilo likatimia.

Kufika chuoni alizidi kupata changamoto na kujiona Maskini kabisa baada ya kujikuta akizungukwa na marafiki ambao wametoka katika Familia zenye uwezo na mafanikio zaidi, na wengi wao walikua wanamiliki vitu vya kifahari na Gharama sana kama Mac Book (Laptop za Apple zenye bei ghali), Simu nzuri Kama "Iphone 6 & Samsung Galaxy Note" pia na kuna wengine walikuwa wanamiliki Magari yao wakiwa mwaka wa kwanza, hivyo basi akiwa kama rafiki tu wakaribu alijaribu kuuficha ukweli na kujifanya na yeye hali ni nzuri tu kama wao ila mwisho wa siku alikuwa anaumia Moyoni kwa sababu alikuwa hawezi kumiliki vitu ambavyo wenzake wanavyo miliki, na kusababisha kujihisi kujitenga na kuto kufanania nao. (Haya yamekuwa maisha ya vijana wengi sana, kuigiza kuishi maisha ambayo kiukweli sio yao).

Baada ya kuona Ndoto zake zote zimekufa na kutokuweza kuishi maisha mazuri aliyoyapenda ndipo alipokutana na malaika ambaye alikuwa ni Kijana Mwanafunzi mwenzake, kwa majina YEKONIA BALIENDEZA ambaye bila uchoyo wowote alimuonyesha Fursa ambayo leo hii imebadilisha kabisa Maisha yake na Mtazamo kiujumla!!

Ali mhabarisha juu ya jinsi atakavyo weza kuishi maisha ya Ndoto Zake na kuwa na uwezo wa kutengeneza Kipato akiwa bado mwanafunzi, Kupitia Kampuni ya kimataifa iliyopo nchi zaidi ya 158 duniani ya Forever Living Products, Na kumfanya ahamasike na kumpa nafasi ya kumuelewesha zaidi, Alishangazwa na jinsi gani alivyokuwa anaifikiria Biashara ya Forever na jinsi alivyo elezewa vilikuwa ni vitu tofauti kabisa na alivyoelewa, alihisi anaijua lakini kumbe alikuwa anaisikia tu! na kuto kuijui vizuri, Baada ya hapo Alielewa Sana na kujiona na yeye tayari ataweza kumiliki Simu nzuri (Iphone 6 Plus), na Kuendesha Gari Lake akiwa bado Mwanafunzi, Alielewa sifa kubwa ya kuwa mjasiriamali ni kutafuta mtaji na hivyo basi alitafuta mtaji kwa nguvu zake zote ili aianze hii Biashara.

Anasema ilikuwa ni Changamoto kuupata mtaji, lakini hakuruhusu kiwe ndiyo kikwazo kwake kufikia maisha ya ndoto zake anayotaka kuyaishi....Aliwaomba Marafiki zake wa karibu, ndugu na jamaa lakini waliishia kumkatisha tamaa, kumcheka na kumvunja moyo, hivyo hakufanikiwa kupata pesa kutoka kwao!!

Lakini bado aliendelea kuota ndoto za maisha anayotaka kuyaishi...na alielewa 'mtaji haujawahi mzuia mtu mwenye ndoto yake ya dhati' hakusikiliza neno la mtu, alikuwa anajua fika anachokitaka! nacho ni kimoja tu "KUFANIKIWA" tu!!

Baada ya kukosa kote alichukua maamuzi magumu ya kuuza Laptop yake ndogo ili apate mtaji wa kuanza hii biashara. Na akafanikiwa kufanya hivyo!!

Safari yake ya mafanikio na Forever Living Products ilianza Tarehe 13 January 2014. Akiwa ameshikwa mkono na Viongozi wake Yekonia Bigirimana Baliyendeza, Lightness Salema na Khushe Hauli

Alifuata kanuni ya Mungu HABAKUKI 2:2 Na Kuandika Njozi zake kwenye Ubao wake wa Ndoto (Dream Board) vile vitu vyote ambavyo alivyokuwa akivitamani ktk maisha yake! na kuamua kufocus na kuifanya hii biashara kwa bidii bila kusikiliza maneno ya watu waliokuwa wanambeza hakupoteza Muda wake, na aliutumia vizuri...kwa kuto kufanya kwa lugha ya kingereza Non Income Generating Activities NIGA (shughuli zisizo muingizia kipato)..na badala yake kufanya shughuli zitakazo muwezesha kuingiza kipato yaani IGA....

Baada ya vipindi na kumaliza ratiba yake ya kujisomea alijitengea muda wakuifanya hii biashara.

NDOTO ZINATIMIA:
Leo hii yupo kwenye Biashara kwa kipindi cha Mwaka Mmoja na Nusu na ameweza kufikia Ngazi ya Manager, ambapo pato lake anapokea walau Tsh Millioni 2 mpaka 4 kwa Mwezi!!

Anaendelea kusema Kupitia Forever living anauwezo wa kutengeneza kipato chenye tija kwa mwezi, na anashukuru mwenyezi mungu kwa kuwa hana tena shida ndogo ndogo kama ilivyokuwa mwanzo!

Ameweza kupanga Nyumba yake, Haishi tena Hosteli, na biashara hii inamuwezasha kulipia pango/ kodi bila Shida!

Ameweza kuwapunguzia wazazi wake mzigo wa kumsomesha, kwa kuwa sasa ana uwezo wa kujilipia ada yake ya Chuo Na Pesa za Matumizi haombi tena nyumbani...

Pia anamshukuru Mungu, Kupitia hii fursa anaishi maisha yenye afya bora, anaishi LIFESTYLE aliyokuwa anatamani kwa wenzake, kwenda Movies Cinema, Swimming, Kuvaa Vizuri na pia kusaidia wengine wenye nia na malengo ya kufanikiwa...
Na pia ameweza Kutimiza Ndoto yake Moja kubwa ya Kununua Simu ya ndoto zake Best Phone (iPHONE 6 PLUS GOLD 64GB).

Anasema Maisha yote aliyoyataka, ambayo alikuwa anayaona kama hayakamatiki na ni ya watu fulani fulani tu! Forever sasa Imeanza kumpatia, na akijiangalia Mpaka ukifika muda wa kumaliza masomo yake ya Chuo atakuwa amepiga hatua kubwa sana ktk maisha yake, kwa uwezo wa Mungu hatakuwa na sababu za kutembeza CV na Kutafuta Ajira tena kama mamillioni ya vijana wengine wanavyofanya na kutaabika na ajira.

Anamalizia kwa kusema Kama Wengine wameweza, Yeye ameweza, basi na Wewe Pia msomaji Unaweza...
Kinachotakiwa ni kuwa na malengo na ndoto unazotaka zitimie ktk maisha yako! na kutafuta nafasi uelezewe kwa undani Kuhusiana na hii Fursa na nini Haswa tunachokifanya!!!

Ahsante!!

Ikiwa umehamasika na ungependa kuchukua hatua kujifunza Biashara

Kwa Maelezo Zaidi Piga: +255 783 149 561 WhatdApp: +255 783 149 561.

0 comments:

Post a Comment