Ofisa
wa Mfuko wa Pensheni PSPF Tawi la Zanzibar Hazina Konde akimkabidhi
msaada wa Magogoro Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Ame Perera
kwa ajili ya Wananchi waliopata maafa ya mvua na kuharibikiwa na mali
zao, makabidhiano hayo yamefanyika katika viwanja vya skuli ya mabanda
ya ngome chumbini Zanzibar.
OFISA
wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Tawi la Zanzibar Hazina Konde akitowa
maelezo kwa niaba ya Mkufugenzi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, wakati wa
hafla hiyo ya kukabidhi msaada wa Magodoro kwa wananchi wa Jimbo la
Chumbuni waliopata janga la mvua za masika katika shehia tatu za jimbo
hilo, Chumbuni. Karakana na Muembemakumbi Zanzibar.
Mbunge
wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Perera Ame Silima akitowa shukrani
kwa uongozi wa Mfuko wa PSPF kwa msaada wao kwa Wananchi wa Jimbo lake
wakati wa makabidhiano hayo yaliofanyika katika viwanja vya skuli ya
mabanda ya ngombe chumbuni Zanzibar.Mhe Mbunge akiishukuru PSPF kwa
kutumia sehemu ya pato lake kwa kusaidia Jamii.
Sheha
wa Shehia ya Karakana Ndg Bakari Makame akitowa shukrani kwa niaba ya
wananchi wake kwa Msaada wa Magodoro yaliotolewa na Mfuko wa PSPF kwa
kujali wananchi wakati wa maafa na
kutowa shukara hizo kwa Uongiozi huo wakati wa makabidhiano ya msaada
huo yaliofanyika katika viwanja vya Skuli ya Mabanda ya Ngome Chumbuni
Zanzibar.
WANANCHI wa Shehia tatu za Jimbo la Chumbuni Zanzibar wakimsikiliza
Ofisa wa Mfuko wa PSPF Tawi la Zanzibar Bi Zahazia Konde akitowa maelezo
kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mfuko huo kwa wananchi wa Jimbo la Chum,buni
Zanzibar wakati wa kutowa msaada wa magodoro kwa wananchi waliopata
maafa ya mvua hivi karibuni.
Wananchi
wa Shehia tatu za Jimbo la Chumbuni Zanzibar wakimsikiliza Ofisa wa
Mfuko wa PSPF Tawi la Zanzibar Bi Zahazia Konde akitowa maelezo kwa
niaba ya Mkurugenzi wa Mfuko huo kwa wananchi wa Jimbo la Chum,buni
Zanzibar wakati wa kutowa msaada wa magodoro kwa wananchi waliopata
maafa ya mvua hivi karibuni.
0 comments:
Post a Comment