Meneja Masoko wa Huwawei Bi
Lydia Wangari, akionyesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) simu
aina ya Huwawei Met 7 ambayo zitauzwa katika Airtel Bazaar linalofanyika
mlimani City ijumaa, jumamosi, na jumapili hii ikiwa na ofa ya simu ya
bure aina ya 'Huwawei Kishkwambi' iliyoshikiliwa na Meneja Masoko wa
Airtel Bi Aneth Muga. Pia simu hiyo itaunganishwa na ofa kabambe ya
kifurushi cha Airtel papo hapo..
Meneja Masoko wa Airtel Bi Aneth Muga akionyesha kwa wanahabari (hawapo pichani) simu ya kisasa ya Airtel Red itakayopatikana kwa gharama nafuu katika Airtel Bazaar litakalofanyika wiki hii ijumaa, jumamosi, na jumapili hii pale mlimani City kwa gharama nafuu hukuikiwa imeunganishwa na kifurushi cha Airtel bure. Anaetazama ni Meneja Masoko wa Huwawei Bi Lydia Wangari.
Meneja masoko wa
Huwawei Bi Lydia Wangari akionyesha kati ya simu mbili zitakazouzwa na ofa ya
'Pata Moja BURE' siku ya ijumaa, jumamosi, na jumapili hii wakati wa Airtel
Bazaar litakalofanyika pale Mlimani City wiki hii. Airtel Bazaar litawawezesha
wateja wa Airtel kujinunulia simu kwa gharama nafuu huku zikiwa zimeunganishwa kifurushi
cha ofa kambambe kwenye mtandao wa Airtel.
---
* Ofa kabambe ya simu za Smart phone kutoka Huawei zikiwa
zimeunganishwa na Airtel
* Simu kuuzwa bei poa zikiwa na ofa za vifurushi kabambe kutoka Airtel
Kampuni ya simu za
mkononi ya Airtel Tanzania ikishiriakiana na Huawei leo imetangaza
kuanza Bazaar lake maalum litakalowawezeha watanzania kujipatia simu za
kisasa za Smart phone na kuweza kufurahia huduma za zote za intaneti
kupitia mtandao wa Airtel
Bazaar la Airtel na
Huawei limepangwa kufanyika kuanzia ijumaa, jumamosi na jumapili hii
kuanzia saa 3asubuhu hadi saa moja usiku katika eneo la ndani la Mlimani
City na litakuwa na muendelezo hapo hapo na baadae litazunguka katika maeneo mbalimbali nchini.
Akizungumzia Bazaar hilo
Meneja masoko wa Airtel Bi Aneth Muga amesema "Bazaar letu litakuwa la
kijanja zaidi kwani simu za smart phone zitakazouzwa ni bora na
zitaambatana na ofa kabambe kuliko zote zinazopatikana sehemu yoyote".
"Mteja wetu uliopo mahali
popote tembelea BAZAAR la Airtel ujinyakulie simu bora na kisasa kama
zile za Huawei au Airtel Red kwa punguzo kabambe zikiwa na kifurushi
cha intaneti kitakachokupa MB 120, SMS 120 pamoja na muda wa maongezi
120 ofa ambapo huwezi kuipata popote zaidi ya kweye Airtel Bazaar" alisema Muga
Meneja masoko kutoka
Huawei Lyidia Wangari aliongeza kuwa licha ya simu za Smart phone za
Huawei kuuzwa kwa gharama nafuu pia atakaenunua simu pale atajipatia
simu nyingine ya bure au zawadi tofauti tofauti papo hapo kwa mfano
"mteja yeyote kati ya 300 wa kwanza kununua simu ya Huwawei aina ya Met 7
DUAL atapata simu aina ya Kishkwambi bure kabisa na atakaenunua simu ya
Huawei Met 7 atapata simu ya bure aina ya Y220 pale pale" alifafanua
Kwa Upande wake Afisa
Airte l wa kitengo cha Smartphone Bw, James Kagashe alisema "tunataka
kudhihirisha kwa wateja wetu kuwa Airtel ndio mtandao sahihi kwa
Smartphone yako popote ulipo, nakuhakikishia kuwa kila simu inayouzwa
katika Artel Bazaar inakuja na ofa kabambe ya kifurushi cha SMS, dakika za muda wa maongezi pamoja na intanet itakayokuwezesha kuperuzi upendavyo"
Nawahamasisha wale wote
mnaotaka kuenda na wakati kwa kumiliki simu bora na kuunganishwa na
mtandao bora kwa Smartphone yako tembelea Airtel Bazaar la Airtel
Mlimani City ili tukuunganishe. Alimaliza kwa kusema Bw Mwanda.
0 comments:
Post a Comment