SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, May 15, 2015

WANAHABARI NA WAMILIKI WA VYOMBO VYA HABARI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WAKUTANA DAR ES SALAAM KUJADILI CHANGAMOTO ZA NCHI ZAO

 Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk. Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungua kongamano la kujadili mchango wa vyombo vya habari katika kuimarisha demokarasia na mambo mbalimbali yanayogusa jumuiya hiyo Dar es Salaam leo
 Mwenyekiti wa Shirikisho la Wafanyabiashara wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Felix Mosha akizungumza katika kongamano hilo.
 Mkurugenzi wa Idara Habari Maelezo, Assa Mwambene akijibu maswali ya wanahabari.
 Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga, akizungumza katika kongamano hilo.
 Wadau wa habari wakiwa kwenye mkutano huo.
 Wimbo maalumu wa Jumuiya hiyo ukiimbwa.
Waziri Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na 
wadau wa habari.
---
Na Dotto Mwaibale

WANAHABARI wa Jumuia ya Afrika Mashariki wametakiwa kukaa pamoja na kuunda sera moja itakayowasaidia kupata habari kutoka pande zote za ukanda huo bila kizuizi.

Mwito huo ulitolewa na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk. Harrison Mwakyembe wakati akifungua kongamano la kujadili mchango wa vyombo vya habari katika kuimarisha demokarasia na mambo mbalimbali yanayogusa jumuia hiyo Dar es Salaam leo.

"Ni jukumu lenu nyinyi wenyewe wanahabri muliopo ndani ya jumuia hii kuanzisha sera moja itakayo wasaidia muweze kufanya shughuli zetu katika nchi yoyoye ya jumuia bila kuzuiliwa" alisema Mwakyembe.

Dk. Mwakyemba alisema serikali haiwezi kuanzisha sera hiyo bali wenye nguvu ya kufanya jambo hilo ni wanahabari wenyewe hivyo ni vema sera hiyo ikiandaliwa waipeleke serikali ili kutengenezwa sheria itakayowapa uhuru waandishi wa jumuia hiyo kufanyakazi zao bila ya kuwekewa na kipingamizi

0 comments:

Post a Comment