SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, May 14, 2015

TRA YAKUTANA NA WADAU KUJADILI SHERIA MPYA YA KODI YA ONGEZEKO LA THAMANI YA 2014 KABLA YA KUANZA KUTUMIKA

 Afisa Kodi Mwandamizi Kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TRA) Bw. Richard Mwafongo akiwasilishaji kwa Taarifa ya Sheria mpya ya Kodi ya ongezeko la Thamani ya mwaka 2014 ambapo  alisema kuwa moja kati ya sababu ya kuandaa sheria hiyo ni kuongeza pato la taifa  kupitia makusanyo mbalimbali wakati wa kikao kilichokutanisha wadau mbalimbali leo jijini Dar es salaam.
 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Rished Bade, akijibu hoja mbalimbali kuhusu Sheria Mpya ya Ongezeko la Thamani  toka kwa wadau waliohudhuria mkutano huo na kuwaasa kuendelea kutoa ushirikiano kuelekea upatikanaji wa sheria hiyo na hatimaye kuwezesha kuinua uchumi wa nchi.
 Afisa Mwandamizi Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Hamisi Lupenja akichangia kwenye moja ya maeneo ya Sheria mpya ya Kodi ya ongezeko la Thamani ya mwaka 2014, wakati wa mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali kujadili maboresho ya sheria hiyo.
 Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Lusekelo Mwaseba  kuendelea kutoa ushirikiano kuelekea upatikanaji wa Sheria hiyo iliyoweza kutumika popote duniani hasa kwenye nchi zinazoendelea itayowezesha ukusanyaji dhabiti wa Kodi na hatimaye kuchangia maendeleo ya nchi.
 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Rished Bade akibadilishana mawazo na baadhi ya washiriki wa Mkutano huo uliofanyika Leo Jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wadau wakichangia kuhusu Sheria mpya ya Kodi ya ongezeko la Thamani ya mwaka 2014.
 Baadhi ya wadau wakichangia kuhusu Sheria mpya ya Kodi ya ongezeko la Thamani ya mwaka 2014
 Baadhi ya washiriki waliohudhuria Mkutano huo wakimsikiliza Afisa Kodi Mwandamizi Kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TRA) Bw. Richard Mwafongo alipokuwa akiwasilisha Taarifa ya Sheria mpya ya Kodi ya ongezeko la Thamani ya mwaka 2014.
Baadhi ya washiriki waliohudhuria Mkutano huo wakimsikiliza Afisa Kodi Mwandamizi Kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TRA) Bw. Richard Mwafongo alipokuwa akiwasilisha Taarifa ya Sheria mpya ya Kodi ya ongezeko la Thamani ya mwaka 2014. Picha na Hassan Silayo-MAELEZO

0 comments:

Post a Comment