SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, May 22, 2015

JE UPO KUNDI GANI KATI YA HAYA?



Kuna makundi manne (4) ya watu wanaotengeneza pesa (KIPATO) hapa duniani.


1. WAAJIRIWA.(EMPLOYEE)
 Hawa ni watu ambao kimsingi wanauza muda wao almost wote wa siku nzima kwa mwajiri wao na yeye anawalipa pesa kwa kuwaambia cha kumfanyia. Kwa kuwa kanuni ya mshahara huwa ni kumlipa mtu 10% ya anachozalisha hasa kwa makampuni makubwa basi haitakaa itokee mwajiriwa kulingana kipato na mwajiri wake. Na hivyo wengi wa waajiriwa hufa maskini na watoto wao pia kuanza kutafuta maisha kivyaovyao kwa kusoma na kuja kuajiriwa pia hivyo hivyo..

2. WALIOJIAJIRI (SELF EMPLOYED) 
Hawa hujitambua kidogo na kuamua kufanya kazi binafsi au kufungua biashara ndogo kama duka nk. Lakini kwa kuwa hawana pesa ya kununua muda wa watu wengine na kuwaajiri hawa nao huwa busy kutwa kucha bila mafanikio ya maana. Ana duka miaka 15 sasa halijawahi kupanuka likawa supermarket. Na mara nyingi huyu mtu akifa na biashara yake nayo humfuata.Sababu kila kitu kinamtegemea yeye.

3. WAMILIKI WA BIASHARA KUBWA (BUSINESS OWNERS)
Hawa huwa na kipato endelevu maana amemunua muda wa watu wengi kawaajiri halafu kawapa majukumu kwa hiyo pesa inamtumikia haitegemei uwepo wake awepo asiwepo pesa inaendelea kuingia kwake. 


4. WAWEKEZAJI (INVESTORS)
Hawa ni watu wenye pesa nyingi zaidi na wana uwezo wa kuiwekeza mahali hata nje ya nchi ikawa inawazalishia pesa zaidi bila wao kuwepo kabisa. 

Kwa hiyo nadhani tayari wewe unajua kundi lipi upo.

SASA SIKIA...
Makundi mawili ya kwanza ni makundi ya watu maskini. Mfano waajiriwa ni watu wanaotumia muda wao na nguvu na maarifa yao yote (waliyoyakusanya kwa miaka mingi ya kusoma kwa shidashida) kumtajirisha mtu kwa malipo kidogo yanayomwezesha huyu muajiriwa kulipa kodi (siyo kujenga), kula, kuvaa, kusafiri kwenda na kurudi kazini nk. Yaani basic needs tu. Maisha ya waajiriwa wengi yanafanana. 

Mfano ni wachache sana katika ajira ambao wamejenga nyumba zao binafsi kwa hela halali ya ajira. Kama vile ilivyo vigumu kwa mwanafunzi kwenda chuo kwa gari lake mwenyewe alilonunua kwa pesa yake halali. Wapo wachache sana. Na hivyohivyo waajiriwa kumiliki nyumba. Wengi wamepanga. 

Waliojiajiri nao wako busy. Kama ana duka basi kufata mzigo yeye (hamwamini mtu), kuuza yeye, usafi yeye, kuhesabu stock yeye, ulinzi wa duka yeye ndo analinda maana analala humo humo. Kama jongoo alivyo na miguu mingi lakini spidi "kiduchu" ndivyo na huyu nae. Miguu mingi ya jongoo bila macho is equal to ZERO.
 Na hivyo hivyo shughuli nyingi bila maarifa is uqual to ZERO. Yaani yuko busy kila saa lakini spidi ya mafanikio ni ndogo kweli kweli. Sasa maendeleo hayaji kwa style hiyo ila kwa kuwa hajui anahisi siku moja na yeye atakuwa kama Bakhressa. Kwani Bakhressa ndo anauza ice cream za Azam?

KWA WANAFUNZI..
Bahati mbaya sana kama ni mwanafunzi uko sekondari au chuo hiyo ndo ramani ya future yako. Ukimaliza chuo lazima uingie katika makundi hayo mawili ya kimaskini hasa kundi la kwanza.


HATA HIVYO.. 
kuna njia ya kukusaidia kuweza kuhama kutoka makundi hayo mawili kwanza na kuingia makundi mawili ya mwisho hapo juu.
Cha msingi ni Wewe kujishusha tu na kukubali kuwa unahitaji kujifunza hivi vitu. Lakini ukifikiri kuwa unajua kila kitu kuna maarifa utayakosa simply kwa kutothamini mawazo ya wengine ambao huenda ni Mungu tu anawaleta ili kukustua kidogo upate ufahamu fulani lakini wewe aaah. Umeziba maskio na pamba umeweka. Uko busy. Uko determined kufa maskini. Hebu jifunze. Itakusaidia. Kama umeajiriwa na unasoma ujumbe huu hebu jiulize ajira yako ikiisha leo ghafla PAAP!! Utaanzia wapi? Kama utaandika CV tena basi kubaliana na hali halisi tu kuwa wewe ni maskini. 


Na kama wewe ni mwanafunzi hii ni habari njema sana maana ukaamua kujifunza vitu hivi sasa hivi ukavifanyia kazi,then I assure you miaka miwili au mitatu mbeleni wakati wenzako wanasambaza CV kuomba ridhaa ya kuingia kundi la kwanza la umaskini wewe utakuwa unanunua gari lako la pili au hata kiwanja na huenda umeanza kujenga kulingana tu na ndoto zako ni zipi.

Tumieni muda mwingi kujifunza haya mambo na siyo kwenda KU-BET timu gani itashinda mechi wiki hii. Unapoteza muda na PESA kwa vitu visivyokujenga. 

Maisha ni mbinu. Kama mpira au kama vita. Mwenye mbinu bora ndio ana win!

Wasiliana Nasi kwa kupiga Simu: +255 783 149 561‬ WatsApp: +255 783 149 561‬ tukupe Mpango Madhubuti wa kubadili maisha yako!

0 comments:

Post a Comment