SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, April 22, 2015

WAZIRI WA FEDHA MHE. SAADA SALUM MKUYA AKUTANA NA BI.SAYEH NA VILEVILE AKUTANA NA MCC/CHAMBER OF COMMERCE

 Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum Mkuya akitoa maelezo ya jinsi Tanzania inavyoboresha uchumi wake kwa Mkurugenzi wa Idara ya Afrika wa (IMF)kwa nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara Bi. Antoinette Sayeh  wa katikati. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha  na Mlipaji Mkuu wa Serikali  Dr. Servacius Likwelile na kushoto ni Gavana wa Benki kuu Prof. Benno Ndulu , akifuatiwa na Gavana msaidizi wa Benki kuu ya Tanzania  Bi. Natu Mwamba
.
 Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum Mkuya wa katikati  akiwa pamoja na ujumbe  kutoka Tanzania walipokutana na ujumbe wa shirikala fedha la kimataifa (hawapo kwenye picha ). Kutoka kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha  na Mlipaji Mkuu wa Serikali  Dr. Servacius Likwelile na kushoto ni Gavana wa Benki kuu Prof. Benno Ndulu , akifuatiwa na Gavana msaidizi wa Benki kuu ya Tanzania  Bi. Natu Mwamba.

 Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum Mkuya akizungumza katika mkutano huo wa Changamoto za Milenia/Chamber of Commerce uliofanyika mjini Washington DC. Aliyeko nyuma ya Mhe Waziri ni Bw. Laston Msongole ambaye ni Mtendaji Mkuu wa mfuko wa milenia wa awamu ya pili

 Bw. Kamran Khan Makamu wa Rais wa shughuli za operesheni  za mfuko wa Changamoto za Milenia akizungumza katika mkutano wa (MCC/Chamber of commerce )akisikilizwa kwa makini na wa jumbe kutoka mfuko wa Changamoto za millennia na Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum Mkuya aliyekaa  mbele.
 Mkurugenzi wa Idara ya Afrika wa IMF kwa nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara Bi. Antoinette Sayeh akiwa na ujumbe kutoka IMF wakizungumza na ujumbe kutoka Tanzania (hawapo kwenye picha).Katika kikao hicho walizungumzia zaidi suala la Tanzania kuzidisha nguvu katika kuboresha sera za kukuza uchumi.

0 comments:

Post a Comment