SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, April 24, 2015

WAZIRI MKUYA AMALIZA ZIARA YAKE NCHINI MAREKANI

Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akiwa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa CITI na Mkuu wa Afrika kwa kundi la sekta ya utumishiwa umma Bw. Peter M. Sullivan alipo mtembelea Mhe.Waziri kwa madhumuni ya kuisadia nchi ya Tanzania katika ubalozi wa Marekani mjini Washington DC.
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya wa katikati akiwa pamoja na ujumbe kutoka Tanzania walipokutana na Mkurugenzi msaidizi na Mkuu wa idara ya Afrika sehemu ya Mashariki Bw.Herve’ Joly walipokuwa wakijadiliana na kuangalia ni jinsi gani Tanzania imeweza kutekeleza sera za Shirika la fedha la Kimataifa mjini Washington DC.
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akimsikiliza kwa makini Bi. Diana Layfield ambaye ni Mtendaji mkuu wa kanda ya Afrika, alipokuwa akieleza mambo ambayo Standard Chartered inaweza kuyafanya katika kuendeleza uchumi wa Tanzania mjini Washington DC.
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akimsikiliza kwa makini Bw. Atlas Mara co-Founder, Ashish. J. Thakkar alipoomba kukutana naye ilikuweza kuangalia jinsi anavyoweza kuja kuwekeza katika nchi ya Tanzania.Mkutano huo ullifanyika mjini Washington DC.Wengine ni wajumbe kutoka nchini Tanzania.
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya alipokutana na Makamu wa Rais JICA anayesimamia nchi za Afrika, Bw. Kato Hiroshi na Bw. Kiyoshi Kodera ambaye ni Makamu wa Rais kiongozi katika Benki ya Dunia, walipokuja kuelezea nia yao ya kutaka kuendelea kuleta miradi nchini Tanzania. Maongezi hayo yalifanyika katika ukumbi wa ubalozi wa Marekani mjini Washington DC.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile akiongoza kikao cha mradi wa kufadhili uwekezaji nyumba. Anayetoa maelezo ni Bw. Baraka kutoka Benki kuu katika mradi huo. Mkutano huo ulifanyika mjini Washington DC.
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile walipokuwa na Naibu katinu Mkuu Marekani Bw. W.L. Mc Donald nje ya jengo la Hazina Marekani.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile na ujumbe kutoka Tanzania walipokuwa wakifanya mkutano wa moja kwa moja kutoka Tanzania na ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali. Kama wanavyoonekana kwenye kivuli cha Runinga.Mkutano huo unafanyka Mjini Washington DC. Na Dar es salaam Tanzania.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile na ujumbe kutoka Tanzania walipokuwa wakifanya mkutano wa moja kwa moja kutoka Tanzania na ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali. Hawapo kwenye picha.Hapa walikuwa wanajadiliana ili wote waafikiane.Mkutano huo unafanyka Mjini Washington DC. Na Dar es salaam Tanzania. (Picha zote na Ingiahedi Mduma Washington DC.)

0 comments:

Post a Comment