Baada
ya mvua ya kama vigudulia kadhaa hili iliyomwagika kwa masaa mawili
mfululizo,maeneo mengi jijini Dar yameungana na bahari ya hindi kwa
kujaa maji na kupelekea adha kubwa kwa wakazi wa jiji hili.Pichani ni
eneo la barabara ya Morogoro.
Matolori ya kuuzia ice cream yakionekana kununiwa leo,huku wapita njia wakiendelea kupiga mbizi kwenye maji hayo.
Barabara ya Bibi Titi Mohamed mambo yalikuwa namna hii,wenye magari madogo walipita kwa staili ya maji ya shingo.
Hapa tena,mwendo wa viatu mkononi.
Kipando nacho kimeroga.
Hapa ndio inakuwaga kimbebe,maana daladala ndio lishabuma tena.
"Hii mvua isharoga tena,na huu mwamvuli miyeyusho kweli".
mvua ikiendelea kupiga.
Hapa dawa ni kutoka nduki tuu...
Hakuna namna nyingine ya kuyakwepa maji haya.hapa ni Posta mpya leo.
Posta mpya mamboyalikuwa hivi
Jamaa wakipiga kibeda Nadia iliyobuma katikati ya barabara,maeneo ya Sinza.
Hapa ni Bamaga leo.
Maeneo ya Kariakoo, hakuendeki kwa muda huu.
Maeneo ya Sayansi ni balaa tupu.
Sayansi....
Kutokana
na mvua kubwa iliyonyesha kwa muda mchache jijini Dar, na kusababisha
kizaa zaa, hivi ndivyo Daladala hili lilivyopotea njia na kuingia
mtaroni huko maeneo ya Gongo la Mboto mchana wa leo.
0 comments:
Post a Comment