MkuuAfisa
Maktaba wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Issa Magabiro akitoa ufafanuzi
kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Bi. Mwantumu Mahiza kuhusu machapisho
mbalimbali yanayotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu leo wakati wa
uzinduzi rasmi wa Semina ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na
Makazi ya Mwaka 2012 mkoani Pwani.
Mkuu
wa Mkoa wa Pwani Bi. Mwantumu Mahiza (aliyekaa) akizindua rasmi
Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 leo
mkoani Pwani. Nyuma yake ni viongozi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu
wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Dkt. Albina Chuwa (kushoto).
Mkuu
wa Mkoa wa Pwani Bi. Mwantumu Mahiza (aliyekaa) akizindua rasmi
Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 leo
mkoani Pwani. Nyuma yake ni viongozi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu
wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Dkt. Albina Chuwa (kushoto).
Baadhi
ya washiriki wa Semina ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na
Makazi ya Mwaka 2012 wakifuatilia masuala mbalimbali leo mkoani Pwani.
Baadhi
ya washiriki wa Semina ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na
Makazi ya Mwaka 2012 wakifuatilia masuala mbalimbali leo mkoani Pwani.
Washiriki
Baadhi ya washiriki wa Semina ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu
na Makazi ya Mwaka 2012 wakiangalia moja ya ramani inayoonyesha
takwimu ya Mgawanyo wa Watu kwa umri na Jinsi na taarifa za Msingi za
Kidemografia, Kijamii na KiuchumI.
Washiriki wa Semina ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 wakiwa katika picha ya pamoja.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
*****************************************
Na. Aron Msigwa –MAELEZO, Kibaha, PWANI.
Ofisi ya Taifa ya Takwimu imezindua rasmi usambazaji wa matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya
mwaka 2012 na kuwataka wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa wilaya na
mikoa kote nchini kuanza kutumia na kuhamasisha matumizi ya takwimu
rasmi zilizotolewa na ofisi hiyo katika kupanga mipango ya maendeleo.
Hayo
yamebainishwa leo mkoani Pwani na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya
Takwimu Dkt. Albina Chuwa wakati akiwakaribisha viongozi, watendaji na
wadau mbalimbali wa mkoa wa Pwani waliohudhuria semina ya usambazaji wa
Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012.
Amesema Tanzania ina takwimu bora kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na Ofisi yake kwa kushirikiana na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuandaa
na kukamilisha taarifa za matokeo ya Sensa yakiwemo machapisho matatu
yanayohusu Idadi ya Watu katika ngazi ya Utawala, chapisho la Mgawanyo
wa Watu kwa umri na Jinsi na chapisho la Taarifa za Msingi za
Kidemografia, Kijamii na Kiuchumi.
Dkt.
Chuwa ameeleza kuwa Ofisi ya Taifa ya Takwimu inaendelea na mikakati
mbalimbali ya kuhamasisha matumizi ya takwimu za matokeo ya Sensa katika
ngazi ya mkoa, wilaya na vijiji ili ziweze kutumika katika kupanga
mipango ya maendeleo.
Ameeleza kuwa takwimu zitakazowasilishwa katika maeneo mbalimbali katinga
ngazi ya kijiji, wilaya na mikoa ukiwemo mkoa wa Pwani ambao umezindua
rasmi shughuli hiyo ya usambazaji wa matokeo zitahusu Umri, Jinsi na
Viashiria muhimu vya umri katika makundi, hali ya ndoa, hali ya uyatima
na vifaa vilivyotumika katika ujenzi wa nyumba .
Amesema
lengo la usambazaji wa takwimu hizo ni kueleza hali halisi ya mafanikio
ya mikoa katika Nyanja za uchumi, umasikini, elimu na afya ili
kuwezesha uboreshaji wa maeneo ambayo hayafanyi vizuri.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Bi. Mwantumu Mahiza akizindua rasmi
Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 kwa ngazi
ya vijiji, Wilaya na mikoa ameeleza kuwa usambazaji wa matokeo hayo utawasaidia na kuwarahisishia viongozi wa maeneo mbalimbali kupanga Bajeti na mipango ya maendeleo.
Amesema
matumizi ya takwimu sahihi yatawezesha upelekaji wa huduma za jamii
zikiwemo shule, hospitali, ujenzi wa masoko, huduma za maji na
kuirahisishia serikali kuwafikishia wananchi huduma hizo kutokana na
takwimu zilizoainishwa katika maeneo husika na kuiepusha serikali
kuwekeza fedha nyingi katika miradi ambayo haiendani na idadi ya watu
katika eneo husika.
Ameongeza
kuwa matumizi ya takwimu hizo kuanzia ngazi ya familia hadi taifa
yatasaidia kupunguza na kuondoa migogoro ya ardhi hususani kurahisisha
suala la umiliki na mgawanyo wa ardhi kulingana na idadi ya watu na
huduma.
Bi.Mahiza
ametoa wito kwa viongozi mbalimbali wa serikali na madhehebu ya dini
kote nchini kuwahamasisha wananchi kutumia takwimu zitakazosambazwa
katika maeneo mbalimbali nchini.
Naye
mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya
watu Duniani (UNFPA) nchini Tanzania Bw.Colins Opiyo akizungumza wakati
wa ufunguzi wa semina hiyo amesema kuwa UNFPA itaendelea kushirikiana na
Tanzania ili kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa na takwimu sahihi.
Amesema
kuwa ili takwimu ziwe sahihi lazima ziendane na uhalisia wa eneo
husika, zitolewe katika muda maalum , zikidhi vigezo vilivyowekwa
kimataifa na kutafsiriwa kulingana na shughuli za kiuchumi za wananchi
wa Tanzania wakiwemo wakulima, wafugaji na wafanyabiashara.
0 comments:
Post a Comment