SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, October 22, 2014

MISS TANZANIA ASHINDWA KUJIBU MASWALI, AACHA MASWALI MENGI YASIYO KUWA NA MAJIBU VICHWANI MWA WATANZANIA, BADO ANA LA KUWAELEZA WATANZANIA WARIDHIKE.1.) BABA MZAZI WA MREMBO HUYO HAJUI MWAKA HALISI ALIOZALIWA MWANAE? MBONA AMEKAA KIMYA?

2.) WAANDAAJI WA MISS TANZANIA HAWAKUWAHI KUJIRIDHISHA NA VIGEZO KABLA YA KUSHIRIKI KWAKE KUANZIA VITONGOJI??, MAANA MOJA YA SHARTI LA MSHIRIKI NI KUONYESHA CHETI CHA KUZALIWA, YEYE ALIONYESHA CHETI GANI HALI YA KUWA ALICHOONYESHA JANA NI KIPYA?

3.) HAO RITA WALIOMTENGENEZEA CHETI KIPYA, WAMEJIRIDHISHA NA NINI HADI KUMTENGENEZEA CHETI KIPYA KINACHOONYESHA TAREHE NA MWAKA WA KUZALIWA UNAOPINGANA NA HATI YAKE YA KUSAFIRIA NA LESENI YA UDEREVA TENA ALIVYOVIPATA KWENYE NCHI ISIYOKUWA NA UBABAISHAJI?

4.) LUNDENGA AMEFUATA VIGEZO GANI NA KUJIAMINI NINI KUWA HATAPATA AIBU NA KUAMUA KUSIMAMA KIDETE KUMTETEA MREMBO HUYO, ATI KUWA MWENYE VITHIBITISHO TOFAUTI NA HIVYO VILIVYOONESHWA JANA ALETE.

5.) MBONA CHETI KILICHO ONYESHWA KATIKA MKUTANO HUO WA JANA NA WAANDISHI WA HABARI NI KIPYA NA CHENYE NEMBO KATIKATI TOFAUTI NA VYETI VYA KUANZIA MIAKA TISINI NA KURUDI NYUMA?
Mzizi wa fitina ukatwe na baba mzazi wa mrembo huyo ajitokeze hadharani kusema ukweli, kuhusu tarehe na mwakwa wa kuzaliwa manawe, ili kama na ye ataongopa kwa kinywa chake Watanzania wamuhuku na kuamini maneno ya watu eti kua ‘’ NI MCHEZO MCHAFU ULIOJULIKANA KUANZAI MWANZO WA USHIRIKI WAKE’’.


Moja ya swali kubwa lililokuwa likimzonga ni kuhusu mwaka wa kuzaliwa kwake ambapo alisema kuwa yeye amezaliwa 31.5.1991 wakati vielelezo vyake mbali mbali alivyokuwa akitumia wakati akiwa nchini Marekani ikiwemo pasi ya kusafiria (passport) na leseni ya udereva ilikuwa ikionyesha amezaliwa 
31.5.1989.

Na kama mshiriki anasema cheti chake kilipotea, ni lini na wapi??? kilipotelea cheti hicho???


Alipotakiwa na waandishi wa habari kujieleza kuwa ni kwanini alikuwa na nyaraka ambazo zilikuwa zinapingana miaka halisi aliyoitaja wakati wa shindano hilo na kusema eti kuwa hayo ni maisha yake binafsi. na kuongeza kuwa 'eti' alipochukuliwa kugombea miss Tanzania wahusika hawakuhitaji vitu kama  pasi ya kusafiria (passport) na leseni ya udereva (driving licence) wao walihitaji cheti cha kuzaliwa tu.Kwa uchunguzi uliofanywa unaonyesha kuwa Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu alishiriki mashindano ya ngazi ya Kitongoji bila ya kuwa na cheti cha kuzaliwa maana mchakato wa kumsaka Miss Chang'ombe mwaka 2014 ulianza Juni 16, 2014 ambapo Mwandaaji wa Mashindano hayo Tom Chilala aliwatambulisha warembo wapatao 17 na Sitti Mtemvu alinyakuwa taji hilo akifuatiwa na Pauline Elisante na wa tatu Darena David.

0 comments:

Post a Comment