SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, October 18, 2014

kuelekea mtanange wa Simba na Yanga, mashabiki milioni 20 matumbo joto

Mega sport.com

Hakuna takwimu sahihi za mashabiki wa klabu kongwe nchini za Simba na Yanga ni wangapi, lakini si chini ya watu milioni 20, akili zao zitasimama kwa takriban dk 90 na kupata kiwewe cha huzuni au furaha wakati miamba hiyo itakapovaana hapo kesho Taifa.

Joto la mechi hiyo tayari limepanda Zaidi ya nyuzi 90 huku kukiwa na hisia tofauti zikiwemo za udanganyifu wa wachezaji kuwa majeruhi ili kuteka akili za wapinzani.

Tayari kuna taarifa Yanga itawakosa wachezaji wake muhimu akiwemo nahodha, Nadir Haroub Canavaro, kiungo mshambuliaji Haruna Niyonzima na Mbrazil Genilson Santana (Jaja) ni majeruhi na huenda wasicheze.
Na kama hiyo itakuwa kweli, basi itakuwa ni kicheko kwa wanamsimbazi kwani kwao itakuwa kama vile kuangusha silaha mikononi mwa waasi.

Simba pia, imetangaza majeruhi wachezaji wake muhimu akiwepo kipa namba moja, Ivo Mapunda, kukiwa na habari kuumia kwake mwezi uliopita kidoleni, huenda asiwe golini na Husein Sharif “Casilas”, kipa mwingine, pia akioonekana majeruhi, akikokotwa katika kiti cha wagonjwa  wakati kikosi cha Simba kiliporejea kutoka Bondeni, Afrika ya Kusini kwa Mzee Madiba.

Yanga inategemea bunduki zake chini ya kocha Mbrazil Marcio Maximo, ambaye yupo nyuma ya kiongozi wa lii (Mtibwa Sugar) akiwa na pointi sita.

Simba, ikiwa chini ya kocha Mzambia Patrick Phiri ambaye, anayejivunia rekodi ya kuchukua ubingwa msimu wa mwaka 1999/2010 bila ya kufungwa, itakuwa na kibarua kigumu cha kufufua matumaini ya mashabikin wake baada ya kuanza ligi kwa kususua, kwa kupata droo tatu ikiwa nyumbani (dhidi ya Coastal Union, Polisi Morogoro na Stand United).
 
Aidha, faraja kwa Simba ni uwezekano wa kuwamo kikosini kwa mshambuliaji wake mahiri,Mganda Emmanuel Okwi, ambaye alisajili akitokea Yanga katika usajili wa dirisha dogo na kuzua mvutano baina ya timu hizo mbili juu ya uhalali wake wa uhamisho. Pia itamtegemea Amisi Tambwe, ambaye ndiye mfungaji bora wa msimu uliopita.

Aidha, kama ilivyo ada ya timu hizo zinapokutana, tayari hisia za uchawi zikiwa zinatawala ili kutafuta ushindi, kama ilivyokuwa katika miaka ya nyuma.
Mara nyingi viongozi wa timu hizi hukanusha tuhuma za kujihusiha na uchawi kwa kudai kuwa ni uvumu na uzushi ambao upande mwingine wa upinzani huutoa ili kuweka akiba kuwa kama watafungwa basi ni kwa njia ya giza.

Kwa kipindi hiki, nazi huwa adimu na silaha kubwa kwa kuumiza upande mwingine huku njiwa wakirushwa na hirizi kufukiwa sehemu za magoli.
Hata utaratibu wa kuingia uwanjani, si ajabu kuvunjwa, kwa wachezaji kutokea katika majukwaa ya mashabiki, tena kwa mafungu.

0 comments:

Post a Comment